Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 0

$
0
0
 Ofisi za Uhamiaji Mkoa wa Njombe

 Wahamiaji Haramu Toka Nchini Ethiopia Wakiwa Katika Ofisi za Uhamiaji Mjini Makambako Kwa Mahojiano Leo

Naibu Kamishina wa Uhamiaji Mkoani Njombe Bi. Rose Mhagama.
 
 Na Gabriel Kilamlya Njombe

 Idara ya Uhamiaji Mkoani Njombe Hii Leo Imewarejesha Nchini Kwao Raia 21 wa  Ethiopia Waliokamatwa Agosti 14 Mwaka Huu Mjini Makambako Kwa Tuhuma za Kuingia Nchini Kinyume cha Sheria Pasipo Kuwafikisha Mahakamani.

Akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Ofisini Kwake Naibu Kamishina wa Uhamiaji Mkoani Njombe Bi. Rose Mhagama Amesema Wameamua Kuwarejesha Kwao Raia Hao Pasipo Kuwafikisha Mahakamani Kwa Kuzingatia Vigezo Mbalimbali Ikiwemo Kupunguza Gharama za Kuwatunza Waethiopia Hao


Naibu Kamishina Huyo wa Uhamiaji Amesema Mara Baada ya Kukamilika Kwa Kuwarejesha Raia Hao Wamiliki wa Gari Lililotumika Kuwasafirisha Waethiopia Hao Ambao ni Kampuni ya Evelest ya Jijini Dar Es Salaam Watachukuliwa Hatua za Kisheria.

Aidha Bi. Mhagama Amesema Kuwa Licha ya Kuwa Jukumu la Kudhibiti Uingiaji wa Raia wa Kigeni Kinyume cha Sheria ni la Serikali Lakini, Naibu Kamishina Huyo wa Uhamiaji Amewaomba Wananchi Kuendelea Kushirikiana na Vyombo Vya Sheria Kuwabaini Watu Wanaojihusisha na

Matukio ya Kuwafarisha Raia Hao.

Raia Hao 21 wa Ethiopia Walikamatwa Agosti 14 Katika Halmashauri ya Mji wa Makambako Ikiwa ni Sehemu ya Raia 46 Waliokamatwa Mkaoni Njombe Tangu Mwezi Disemba MWaka Jana Hadi Sasa Huku Idadi Kubwa ya Raia Hao ni Kutoka Nchi ya Ethiopia Wakiwa na Lengo la Kufika Nchi za Afrika Kusini na Malawi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles