MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE Wajadili Taarifa ya CAG
Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bi.Rhoda Mahava.
MADIWANI WA HALMASHAURI WAKIJADILI MADA MBALIMBALI ZA UTEKELEZAJI WA MIRADI KATIKA KATA ZAO
JULIUS SALINGWA NI DIWANI WA KATA YA KIDEGEMBYE AKIZUNGUMZA
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE PAUL MALALA AKISOMA MUHTASARI WA MKUTANO ULIOPITA
MAKAMU MWENEYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE AKITETA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE
PIKIPIKI ZILIZOKABIDHIWA KWA KATA MBILI MTWANGO NA MATEMBWE ZILIZOTOLEWA NA SHILIKA LA TASSF KAMA ZAWADI KWA USHINDI WA USAFI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Licha ya Jitihada Kubwa Zilizofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe za Kuongeza Ajira Kwa Watumishi Wapya Mara Baada ya Kupata Kibali Cha Ajira na Kufanikiwa Kuajiri Watumishi 177 Kwa Mwaka 2013/2014 Lakini Bado Inakabiliwa na Upungufu wa Watumishi 156.
Kutokana na Hali Hiyo Halmashauri Hiyo Imeendelea Kujiwekea Mkakati wa Kufuatilia Vibali Vya Ajira za Watumishi Wengine Ili Ifikapo Disemba 31 Mwaka Huu Suala Hilo Liwe Limefanikiwa.
Akitoa Taarifa Kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Kwenye Kikao Maalumu cha Madiwani Cha Kujadili Taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Mweka Hazina wa Halmashauri Hiyo Bi.Rhoda Mahava Amesema Kuwa Halmashauri Hiyo Imelazimika Kuajiri Watumishi Wapya wa Sekta Mbalimbali Baada ya Kupewa Kibali na Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Bi.Mahava Amesema Kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Ilipaswa Kuwa na Watumishi 2107 Ili Kukidhi Matakwa ya Upungufu wa Watumishi Katika Halmashauri Lakini Baada ya Taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Kubaini Tatizo Hilo Iliagiza Kutolewa Kwa Ajira Kwa Watumishi Hao Jambo Ambalo Hadi Sasa Imekwisha Ajira Jumla ya Watumishi Hao 177 Kati ya 333 Waliotakiwa Kuongezwa.
Pamoja na Mambo Mengine Halmashauri Hiyo Imerejesha Hazina Kuu Zaidi ya Shilingi Milioni 50 Fedha Ambazo Hazikutumika Kama Mishahara ya Watumishi Mbalimbali Wakiwemo Waliostaafu,Watoro,Waliofariki na Walioacha Kazi Jambo Ambalo ni Kinyume Cha Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Serikali za Mitaa ya Mwaka 2009.
Akijibu Baadhi ya Maswali ya Madiwani Katika Kikao Hicho Waliotaka Kujua Hatua Zinazochukuliwa Dhidi ya Ubadhilifu Unaotokana na Uzembe wa Baadhi ya Watumishi Serikali Mkaguzi Huyo Amesema Kwa Kawaida Taarifa Zinawasilishwa Bungeni Kwa Majadiliano Ambako Ndiko Hatua Zaidi Huchukuliwa na Wabunge Kutoa Maagizo Kwa Serikali.