Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 2

$
0
0

USAILI WA JESHI LA POLISI TANZANIA KWA WAKAZI  wA MBEYA

 Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, BARAKAEL .N. MASAKI –

ACP anawatangazia Wananchi wote ya kuwa orodha ya majina ya vijana

waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2013 na cha Sita mwaka 2014 na

kuchaguliwa kufanya usalii wa kujiunga na Jeshi la Polisi inapatikana

kwenye tovuti ya Polisi: www.policeforce.go.tz au wafike ofisi

ya kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya iliyopo Forest jirani na

Mahakama kuangalia majina yao.

Muhimu:
 

•Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha

usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe zinavyoonesha kwenye

jedwali hapo juu ili mradi tu awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa

walioitwa kwenye usaili. Jeshi la Polisi halitahusika na lawama yoyote ile

kwa mtu atakayekwenda kwenye kituo cha usaili hali ambapo jina lake si

miongoni mwa walioitwa kufanya usaili.




• Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya

masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s)

], nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya

kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.




• Mwombaji awe na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo

atachaguliwa..

 

• Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula

na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. Pia waombaji waje na

kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.

Ni muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia muda wa kuanza usaili.





TAREHE YA USAILI KWA MKOA WA MBEYA NI 28.09.2014 HADI

01.10.2014. SAA 08:00 ASUBUHI HADI 10:00 JIONI.
mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmm


Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles