Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

KAFULILA ALITAKA KUMVURUGA MAKINDA BUNGENI LEO JUU YA AKAUNTI YA ESCROW NA IPTL

$
0
0
Sakata la Mbunge David Kafulila na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Fredrick Welema Juu ya Akaunti ya ESCROW na IPTL Lilitaka Kutikisa Bunge Leo Asubuhi Baada ya Mbunge Huyo Kuwasha Moto Mwingine kwa Lengo la Kutaka kufahamu hatua zilizochukuliwa baada ya kuwasilisha Nyaraka Alizotakiwa kuziwasilisha kwa uchunguzi zaidi.
 
Katika Kikao cha Bunge la Bajeti hii leo Bungeni mjini Dodoma  Kafulila Aliomba Muongozo wa Spika Ili afahamu Muenendo wa Sakata Hilo la Tuhuma za Ufisadi wa Takribani shilingi Milioni 200 lakini Mbinu hiyo Imegonga Mwamba baada ya Spika Kumkandia na Kumtaka Kuacha Tabia ya Kutangaza Kila Jambo Kwenye Vyombo Vya Habari.

Spika Anne Makinda Amesema Tabia ya Mbunge Huyo Kukimbilia Kwenye Vyombo vya Habari Kueleza Hali ya Sakata Hilo Ilihali Tayari Bunge limeshatoa Maagizo ni utovu wa Nidhamu.

Aidha Makinda Amelazimika Kuizima Hoja Hiyo Kwa Kusema Kesi Hiyo Itafanyiwa Kazi na TAKUKURU na Si Bunge Tena hivyo Haina Haja ya Kuendelea Kuijadili Ambapo Pamoja na Mambo Mengine Mbunge Kafulila Alilalamikia Hatua ya Kutishiwa na Jaji Welema

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles