Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 1

$
0
0

WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI NJOMBE KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MLINZI.

Jeshi la polisi mkoani Njombe linawashikilia watu watatu kwa mahojiano zaidi kuhusu mauaji ya mlinzi aliyekutwa amekufa mkoani hapo. 

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kusainiwa na kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani imemtaja Bw. Abdul Kiswaga (49) mkazi wa kitongoji cha Ramadhani kata ya Njombe mjini, kuwa amekutwa akiwa ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mtu ama watu wasiofahamika. 

Taarifa hiyo imesema tukio hilo limetokea Juni 3 mwaka huu ambapo mwili huo wa marehemu ambaye alikuwa mlinzi umekutwa katika mtaa wa Msikitini kata ya Njombe mjini. 

Wanaokamatwa kwa maojiano kuhusu mauaji hayo ambao nao ni walinzi ni pamoja na Stephano Msasi (25) mkazi wa Uyelevale, Jacob Fungamila (22) mkazi wa Uyelevale na Julius Mwangande (55) mkazi wa Msikitini Njombe. 

Aidha mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Kibena Njombe na kiini cha mauaji hayo bado kinachunguzwa 
Chini ni Picha za Matukio ya Mauaji ya Mlinzi Huyo Yaliyotokea Usiku wa Kuamkia Juni 3 Mjini Njombe Katika eneo la Uchochoro wa Nyumba ya Kulala Wageni Ya AMANI LODGE Mkabala na Kituo Cha Mafuta Mjini Njombe

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles