Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 3

 Mwili wa Mlinzi aliyefahamika kwa jina Moja la Kiswaga Ukiwa Chini ya Uchochoro karibu na Nyumba ya Kulala wageni ya Amani Lodge Mjini Njombe Asubuhi ya Leo



Image may be NSFW.
Clik here to view.

 Polisi Wakiwa Eneo la Tukio Mapema Leo
 Katikati n mlinzi aliyejaribu kupambana na majambazi hao hadi kuchaniwa Suruali ya Kazi lakini wakafanikiwa kutokamea kusiko julikana



 Mwili wa marehemu adamu kiswaga aliyeuwa katika lindo ukipelekwa hospitali



Hii ni taswira ya Mji wa Njombe Ambako Matukio ya Mauaji Yamekuwa Yakijitokeza 

Na  Gabriel Kilamlya Njombe

 Mlinzi wa Maduka Matatu Mjini Njombe Adamu Kiswaga  Mwenye Umri Kati ya Miaka 45-50

Ameuawa na Watu Wasiofahamika Usiku wa Kuamkia jana akiwa katika eneo lake la kazi

Tukio Hilo Limetokea Majira ya Saa Nane Usiku Katika Eneo la Nyumba ya Kulala Wageni ya

Amani Lodge Mkabala na Kituo Cha Mafuta Cha GAPCO Ambapo Mlinzi Huyo Ameuawa na Kitu

Kizito Kichwani Wakati Akiwa Lindoni.

Wakizungumza na www.gabrielkimlya.blogspot,.com Baadhi ya Mashuhuda na Walinzi Waliokuwepo Katika Eneo la

Tukio Wamesema Kuwa  Mlinzi Huyo Ameuawa na Watu Wawili Ambao Hawakuweza

Kuwatambua Wakati Wakitaka Kujaribu Kubomoa  Nyuma ya duka la Mzee Makete Kwa Lengo
 
la Kutaka Kuiba mali zilizomo katika duka hilo

Aidha Baada ya Kumuuwa Mlinzi Huyo Ndipo Walipotaka Kuanza Kubomoa Jengo Hilo na Kisha

Kukutana na Walinzi Toka Maeneo Mengine na Waka  pambana Nao Pasipo Silaha za Moto Kisha

Watu Hao Wanaodhaniwa Kuwa ni Majambazi Wakapata Mwanya wa Kutoroka.

Baadhi ya Wahudumu na Wateja Waliolala Katika Nyumba Hiyo ya Amani Lodge Wamesema

Kuwa Mara Nyingi Walinzi Katika Eneo Hilo Wamekuwa Wakiota Moto Nyuma ya Nyumba Hiyo

Katika Jiko la Kuchemshia Maji huku wakiacha malindo yao bila ulinzi.

Rodgers Mhagama ni Mmoja wa Waajiri wa Mlinzi Huyo Katika Maduka Hayo Ambaye Amesema

Kuwa Mlinzi Huyo Alikuwa Akilinda Kwa Kutumia Silaha za Jadi  Hali Iliyosababisha Mlinzi Huyo

Kuzidiwa Nguvu.

Hadi kamera ya mtandao huu Ikiondoka Katika Eneo la Tukio Jeshi la Polisi Lilikuwa Limefika na Kuchukua Mwili wa Marehemu Huyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles