Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

WAKAZI NJOMBE WALIA KUCHELEWESHWA KWA BAJETI TOKA SERIKALI KUU,WAMUOMBA SPIKA ANNE MAKIINDA AANZA KUTAZAMA HILO KWENYE BUNGE LA BAJETI

$
0
0
Spika wa Bunge Anne  Makinda
Na Gabriel Kilamlya Njombe.

Baadhi ya Wanasiasa na Viongozi Mbalimbali Mkoani Njombe Wamekuwa na Maoni Tofauti Juu ya Bunge la Bajeti Lililoanza Rasmi Leo,Kutokana na Serikali Kushindwa Kukamilisha Upelekaji wa Fedha Za Miradi Ya Maendeleo Katika Halmashauri Mbalimbali Hapa Nchini.

Wakizungumza na Tovuti hii Kwa Nyakati Tofauti Mjini Njombe Baadhi ya Wanasiasa Hao Wamesema Kuwa Kitendo cha Serikali Kuruhusu Kuanza Kwa Bunge la Bajeti Ya Mwaka 2014/2015 Ilihali Bajeti ya Mwaka Unaoisha Mwezi Juni Mwaka Huu Kushindwa Kutekelezeka Kwa Asilimia Kubwa ni Kuongeza Mzigo wa Matatizo Kwa Wananchi.

Baadhi ya Wanasiasa Hao Waliozungumza na Kituo Hiki ni Pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha TLP Wilaya Ya Njombe Ambaye Amesema Kuwa Bunge Hilo Linaonekana Kuwa Kero Kwa Watanzania Kutokana na Bajeti Ya
Mwaka 2013/2014 Kufanya Kazi Tofauti na Malengo Yaliyokuwepo.

Alatanga Nyagawa ni Kaimu Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Njombe Ambaye Amesema Kuwa Licha ya Kuwepo Kwa Makadilio Ya Shilingi Trilioni 19.6 ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha Ujao Lakini Imeonekana Bajeti Hiyo Imekuwa Ndogo Kulingana na Majukumu Makubwa Ya Serikali Yanayotarajiwa Kufanyika Katika Siku Zijazo.

Miongoni Mwa Mambo Hayo Amesema ni Pamoja na Mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu,Mchakato wa Uundwaji wa Katiba Pamoja na Suala la Uandikishwaji wa Vitambulisho Vya Uraia.

Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Halmashauri Ya Mji wa Njombe Bwana Edwin Mwanzinga Amesema Kuwa Licha ya Vikao Hivyo Vya Bunge la Bajeti Kufanyika Kwa Mujibu wa Sheria Lakini Bado Taifa Litaendelea Kushindwa Kutekeleza Miradi ya Kimaendeleo Kutokana na Bunge Hilo Kuendelea Kuwa la Makasio na Makadirio.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles