Baadhi ya Wafanyabiashara Wakiendelea Kuchangamkia Biashara Zao Katika Msimu Huu wa Siku Kuu Ya Pasaka
Na Jema Mgungile Njombe
Katika Kile Kinachodaiwa ni Kumlinda Mteja Wakati wa Msimu Huu Wa Siku Kuu Ya Pasaka,Wafanyabiashara Mjini Njombe Wamesema Hawatoongeza Bei Ya Bidhaa Zao Sokoni.
Hatua Hiyo Imekuja Kufuatia Kuwepo Kwa Ukali wa Maisha na Kupanda Kwa Gharama za Maisha Na Hivyo Kwa Upande wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu Mjini Njombe Wamesema Hawatopandisha Bei Ya Bidhaa Zao Ili Kutompoteza Mteja.
Wakizungumza na Uplands Radio Baadhi Ya Wafanyabiashara Sokoni Hapo Wamesema Kuwa Imekuwa ni Kawaida Kupandishwa Kwa Bei Ya Nafaka na Bidhaa Mbalimbali Katika Msimu wa Siku Kuu Lakini Kwa Mwaka Huu Hawatopandisha Bei Kutokana na Kupanda kwa Gharama ya Maisha.
Hata Hivyo Wamesema Kuwa Endapo Kutakuwa na Mabadiliko Yoyote Ya Gharama za Bidhaa Sokoni Hapo Basi ni Lazima Wafanyabiashara Hao Watatangaziwa Kwa Utaratibu Maalumu.
Pamoja na Mambo Mengine Wamewatoa Wasiwasi Wateja Juu Ya Gharama za Bidhaa Mbalimbali Sokoni Hapo na Kwamba Katika Siku Kuu Hii Ya Pasaka Wananchi Wanapaswa Kwenda Sokoni Hapo Kupata Bidhaa Mbalimbali Kwa ajili ya Maandalizi Ya Siku Kuu Hiyo
Kumekuwepo na Utaratibu wa Kupandisha Bei Ya Vitu Mbalimbali Katika Msimu wa Siku Kuuu Mbalimbali Hapa Nchini Kitu Ambacho Husababisha Kuibuka Kwa Malalamiko Miongoni Mwa Jamii Mkoani Njombe.
...................................................................................................................................