Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 7

$
0
0

TANESCO NJOMBE WANASA MAJAMBAZI WA NYAYA ZA UMEME Power station


















 HAWA NDIO VIJANA WALIOHUSIKA NA WIZI WA NYAYA ZA UMEME MJINI NJOMBE na Mmoja ametokomea kusiko julikana
















Na Gabriel Kilamlya  Njombe

Shirika la Umeme Tanesco Wilaya ya Njombe Leo Limefanikiwa Kuwanasa Watu Wawili Waliokutwa Wakiiba Nyaya za Umeme Katika Kituo cha Kusambazia Umeme Yaani Power Station Mjini Njombe Huku Wawili Wakihusika Katika Tuhuma Tofauti Ikiwemo Ya Kununua Nyaya Hizo na Mmoja Kushindwa Kuwajibika Kama Mlinzi wa Zamu.

Tukio Hilo Limetokea Majira ya Saa Nne Asubuhi Huko Katika Mtaa wa Uzunguni Kwenye Kituo Hicho cha Umeme Yaani Power Station Ambapo Vijana Wawili Wamekatwa na Mmoja Ametokomea Kusiko Julikana Wakati Wa Msako Huo.

Akizungumza Mara Baada ya Kuwafikisha Kwenye  Kituo cha Polisi Mjini Njombe Msimamizi wa Shirika la Umeme Wilaya ya Njombe Bwana Renatus Henerico Amesema Kuwa Wizi wa Nyaya Hizo Ulianza Tangu Wiki Iliyopita Lakini Kutokana na Kuweka Mtego wa Kuwanasa Wezi Hao Leo Zoezi Hilo Limefanikiwa.

Bwana Renatus Amewataja Watuhumiwa Hao Kuwa ni Pamoja na Justin Kyando Mwenye Umri wa Miaka 17 Mkazi Wa Ramadhani Mjini Njombe,Gehazi Kilumbe Mwenye Umri wa Miaka 18 Ambaye naye ni Mkazi wa Mtaa Huo wa Ramadhani,Felista Ngota Ambaye ni Mnunuzi wa Nyaya Hizo Pamoja na Anna Mhenga Ambaye Alikuwa Mlinzi wa Zamu Katika Lindo Hilo.

Aidha Amemtaja Castory Mligo Kuwa Ametoroka wakati Wa

Tukio Hilo na Kwamba

Miongoni Mwa Vijana Hao Wawili Walikuwa Wafanyakazi wa Mkataba Mfupi Katika

Shirika Hilo Yaani S.T.E Ambapo Baada ya Mkataba Wao Kuisha Wakaanza Kujihusisha

na Matukio Hayo.

Pamoja na Mambo Mengine Amesema Kuwa Nyaya Hizo Zilizo Ibiwa Hadi Sasa

Zinagharimu Zaidi Ya Shilingi Milioni 60 Kwani Walianza Kuiba Tangu Siku Nyingi.

Upands Radio Imefanikiwa Kuzungumza na Mmoja wa Watuhumiwa Hao Anayefahamika

Kwa Jina la Justin Kyando Ambaye Amesema Kuwa Wamekuwa Wakiiba  Nyaya Hizo na

Kuziuza Kwa Mfanyabiashara Huyo Felista Ngota Ambaye ni Mnunuzi wa Vyuma Chakavu

Katika Mtaa wa Msichoke Mkabala na Chuo Kikuu cha Amani Mjini Njombe.


Bwana Christian Mlelwa ni Mkuu wa Ulinzi Katika Kampuni Ya Jirani Security Group

Yenye Makao Makuu Yake Jijini Dar es Salaam Ambaye Amesema Amekuwa Akimuomba

Mkurugenzi wa Kampuni Hiyo Kumuongezea Walinzi Hususani Katika Eneo Hilo la Power

Station Lakini Hakuna Utekelezaji Wowote Kwani Eneo Hilo ni Kubwa Zaidi.

pichani ni Msimamizi Mkuu wa Shirika la Umeme la Tanesco Wilaya ya Njombe Bwana Renatus  Henerico Akizungumza na mtandao huu kufuatia tukio hilo hii leo.
HayA Ndio maganda ya waya Huo Baada ya Kuchunwa na Wezi hao

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles