Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 12

$
0
0

BONGO MOVIE YAPATA PIGO JINGINE.




Muigizaji wa filamu nchini Jaji Khamis (Kashi) amefariki dunia leo  mchana  katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.


Kashi amewahi kutamba na mchezo wa ITV, Tamu Chungu akiwa na wasanii wenzake kama Mzee Masinde,Samson na wengine.

Baada ya kupata habari hii, mwandishi wetu aliongea  na muigizaji mwenzake Monalisa ambae amethibitisha kutokea kwa msiba huo. Monalisa amesema alipata taarifa jana kwamba Kashi amelazwa hospitali akiwa amezidiwa kiasi cha kushindwa kuongea na hivyo kushindwa kujua nini kilikuwa kinamsumbua.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles