Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

MKOA WA NJOMBE WAPATA WALIMU WAPYA 831 AJIRA MPYA

$
0
0
Na  Festo James  Njombe

Katika Kuhakikisha Tatizo la walimu wa shule  za Sekondari na Msingi  linaendeleaa

kuatatuliwa,  Mkoa wa Njombe  Umepokea  Walimu Zaidi ya Mia Nane  Ambao

Wameanza Kuripoti Katika  Vituo Vyao vya Kazi  Tangu Hapo Juzi.

Akiongea na Kituo Hiki  Afisa Elimu Mkoa wa Njombe  Bw Said Kinyaga Nyasiro 

Amesema Kuwa Kati ya Walimu Hao walopangwa katika Mkoa wa

Njombe ni walimu

831 Ambapo Walimu wa  Masomo ya Sayansi ni  54 huku walimu wa sanaa ni  walimu

ni  445  na walimu wengine  ni wa cheti   wakiwa 332 .

Katika Hatua Nyingine  Afisa Elimu Huyo Amewashauri wadau wa Elimu  Pamoja na

Wananchi  Mkoani Njombe  Kutoa Ushirikiano  Wa Kutosha na  Kutokuwakatisha  

Molali Walimu Wapya  waliopangiwa  ambao wanatarajia Kuanza   Kutoa Elimu Katika

Mkoa wa Njombe.

Aidha Afisa Elimu Huyo Amebainisha Kuwa  Walimu 179 wanaratajia Kwenda Wilaya

Ya Makete,132 Wilaya ya Ludewa, 127 Wilaya ya Wanging'ombe na Wilaya ya Njombe

Walimu 393 Watakao Sambazwa Kwenye Halmashauri Zake.

Bw Nyasiro   Ameongeza Idadi Hiyo ya Walimu imekuja wakati Mkoa wa Njombe Ikiwa

na Upungufu wa Walimu  Zaidi ya Elfu Mbili  Hivyo Kuwataka Walimu Hao wapya

Kuwasili Katika Vituo Walivyopangiwa Mapema Kama Sheria Inavyosema.


Ameongeza Kuwa Mapokezi Hayo ya Walimu Yanaenda Sanjari na  Uhakiki  wa  Uhalali 

 wa Walimu Hao Kwa Kuachunguza Vyeti Vyao.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles