Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 0

$
0
0

WIKI YA UPANDAJI MITI KITAIFA WAFANYIKA KIBENA NJOMBE,JAMII YAASWA KUJIKITA KATIKA UWEKEZAJI WA MITI

pichani ni katibu tawala Mkoa wa Njombe Bwana Jackson Saitabau Akisoma taarifa ya Hali ya Utunzaji mazingira Mkoani Njombe

Mkuu wa mkoa wa Njombe Keptain Mstaafu Aseri Msangi Amewataka wananchi na  taasisi za sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika zoezi la upandaji wa miti rafiki kwa vyanzo vya maji na miti ya mbao katika kwa maeneo mengine yanayostahili kupandwa huku akiwatahadharisha na matukio ya moto kichaa na ukataji ovyo.

Aidha Keptain mstaafu Msangi pia amerejea kauli yake ya kuwataka wananchi kupanda miti ya matunda ili iwasaidia kutatua tatizo la kifedha miongoni mwa wananchi na sekta binafsi jambo litakalosaidia kutokatwa kwa miti kabla ya wakati wake ambapo pamoja na mambo mengine wametakiwa kukata mti na kupanda mti kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyojieleza.

Akizungumza na wananchi wa mitaa ya Kibena Keptain Msangi amewapongeza wananchi na taasisi binafsi zinazostawisha vitaru vya miche ya miti na kuwataka kutambua umuhimu wa miti hiyo kuwa ni sehemu ya zao huku akiwaagiza viongozi wote wa vijiji na kata kuhakikisha wanalisimamia tatizo la moto kichaa pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi na mapema kuuzimisha moto utakao kuwa umejitokeza maeneo yao.

Hata hivyo amesema kuwa jitihada za kupanda miti zinatakiwa kwenda sambamba na ufugaji wa nyuki katika maeneo hayo huku akiyataka makapuni Na taasisi mbalimbali yaliopo mkoa wa Njombe ikiwemo kampuni ya  Tanwat kuhakikisha inaendeleza kupanda maeneo mengine ambayo hayajapandwa miti kwenye vyanzo vya maji.

Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii bi.Maimuna Tarishi akisoma taarifa ya

Wizara  ya Maliasili na Utalii amesema kuwa kumekuwapo na ongezeko la upandaji wa

miti kwa mwaka 2005 na 2006 hadi 2012 na 2013  takwimu zinaonesha wastani wa

miti milioni  mia moja sitini na tano kwa mwaka sawa na asilimia sitini na tano ambayo

inaendelea kukua mpaka sasa maeneo mbalimbali hapa nchini.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Edwin Mwanzinga Akizungumza Kwenye Kilele cha Upandaji miti Leo.

Na Michael Ngilangwa Njombe

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe bwana Edwin Mwanzinga amesema

kuwa halmashauri ya mji wa Njombe itaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya

upandaji na utunzaji wa mazingira hususani kwenye vyanzo vya maji pamoja na

matukio ya moto kichaa.

Kwa upande wao wananchi na viongozi wa mitaa ya Kibena wamesema kuwa jitihanda

za upandaji miti  kwenye vyanzo vya mazingira zimekuwa zikiendelea kila maeneo lakini

wanasikitishwa na kampuni ya Tanwat kushindwa kuondoa miti isiyo rafiki kwenye

vyanzo vya maji jambo linalosababisha wananchi kukosa maji msimu wa kiangazi

kutokana na vyanzo vyake kukauka.

Kauli mbiu ya mwaka Huu inasema Miti ni Uhai Panda miti kwanza  Ndipo Ukate Mti 

ambapo mkoa wa Njombe umepongezwa kwa hatua kubwa ya kupanda miti kwa wingi

na kuwataka wananchi na taasisi kuendelea kupanda miti hiyo kwa manufaa yao.
..........................................................................................................................................

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles