Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Akikabidhiwa Misaada Toka Kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya TANWATT Kibena Dokta Rajeev Singa Kulia Kwa ajili ya Ukarabati wa Shule ya Msingi Kibena.
Hivi ni Baadhi ya Vifaa Vilivyotolewa na Kampuni ya Miwati ya TANWATT Kibena Njombe Kwa Ajili ya Kusaidia Ukarabati Mdogomdogo Katika Madarasa Ya Shule ya Msingi Kibena.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kibena Mwl.Meshack Mnyawasa Kulia Akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Wakizungumza Jambo Bada ya Kukabidhiwa Misaada Toka Kampuni ya Tanwatt Mjini Njombe.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Akizungumza na Wanafunzi wa Shule Ya Msingi Kibena Leo Alipofika Shuleni Hapo.
Hawa ni Wanafunzi Katika Shule ya Msingi Kibena Wakiwa Darasani Wakiwa Kwenye Jengo Ambalo Linatajwa Kuwa Linauafadhali.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Akisoma Jiwe la Msingi la Shule ya Msingi Kibena Lililozinduliwa na Hayati Julius Nyerere Mnamo Mwaka 1956 August 4,Shule Ambayo Hadi Sasa Imeonekana Kuchakaa Kwa Majengo Yake.
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Ameiagiza Halmashauri ya Mji wa Njombe Kuhakikisha Inafanya Tathmini ya Uchakavu wa Majengo Katika Shule ya Msingi Kebena Ili Yaweze Kufanyiwa Ukarabati Mkubwa.
Bi.Dumba Ametoa Agizo Hilo Wakati Akipokea Misaada ya Vifaa Mbalimbali Iliyotolewa na Kampuni ya MIWATI ya Kibena TANWATT Kwa Ajili ya Ukarabati wa Baadhi ya Majengo ya Shule Hiyo Kutokana na Uchakavu Uliokithiri Shuleni Hapo.
Aidha Mkuu Huyo wa Wilaya Pia Ameziagiza Kamati za Ujenzi , Ikiwemo Kamati ya Shule ya Msingi Kibena Kuhakikisha Zinafanya Ukarabati Mdogo wa Baadhi ya Madarasa ya
Shule Hiyo Ili Kuepusha Majanga Yanayoweza Kujitokeza Kutokana na Mvua Zinazoendelea Kunyesha.Bi.Dumba Ametoa Agizo Hilo Wakati Akipokea Misaada ya Vifaa Mbalimbali Iliyotolewa na Kampuni ya MIWATI ya Kibena TANWATT Kwa Ajili ya Ukarabati wa Baadhi ya Majengo ya Shule Hiyo Kutokana na Uchakavu Uliokithiri Shuleni Hapo.
Aidha Mkuu Huyo wa Wilaya Pia Ameziagiza Kamati za Ujenzi , Ikiwemo Kamati ya Shule ya Msingi Kibena Kuhakikisha Zinafanya Ukarabati Mdogo wa Baadhi ya Madarasa ya
Katika Hatua Nyingine Bi. Dumba Amewataka Viongozi wa Mtaa Huo Kuwahamasisha Wazazi na Walezi Ili Waweze Kutambua Kuwa Shule Hiyo ni Mali Yao na Kuondoa Dhana ya Kuwa Shule Hiyo ni Mali ya Serikali Hali Inayosababisha Baadhi ya Wananchi Kukaidi Kuchangia na Kuitunza Shule Hiyo.
Akiongea Wakati Akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Kwaniaba ya Uongozi wa Shule ya Msingi Kibena ,Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanwatt Kibena Dokta Rajeev Singa Amesema Vifaa Hivyo Vinathamani ya Shilingi Milioni 1.9 Kwa Ajili ya Kusaidia Ukarabati Shuleni Hapo na Kuongeza Kuwa Wataendelea Kusaidia Katika Shughuli Mbalimbali za Kijamii Kwa Mujibu wa Mikata Inavyowataka Wawekezaji Mbalimbali.
Awali Katika Taarifa Fupi Ya Shule Hiyo Iliyosomwa na Afisa Mtendaji wa Mitaa ya Kibena Otmary Daniel Mbangala Imeeleza Kuwa Uchakavu wa Shule Hiyo Umetokana na Kuwa Shule Hiyo Imejengwa Muda Mrefu Kwani Hadi Sasa Ina Miaka 58.
Shule ya Msingi Kibena Ilijengwa Mnamo Mwaka 1956 na Kuanza Rasmi Mwaka 1964 Baada ya Kuzinduliwa na Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere na Hivyo Hali Hiyo Imesababisha Kuwepo Kwa Kiwango Kikubwa cha Uchakavu wa Madarasa Yanayohitaji Ukarabati Mkubwa.