Baadhi ya Wasanii Wakiwa Kwenye Kikao cha Kwanza cha Maandalizi ya Matamasha ya UMOJA KWANZA Kupitia Kituo cha Radio cha UPLANDS FM Njombe.
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Wasanii wa Michezo na Nyimbo Mbalimbali Wilayani Njombe Wameanza Kushiriki Vikao Vya Maandalizi ya Matamasha ya UMOJA KWANZA Yanayoandaliwa na Kituo cha Radio cha Uplands Fm Kilichopo Mjini Njombe.
Kwa Mujibu wa Mwenyekiti wa Matamasha Hayo Bwana James Eugen[Dj Quest The Best] Ameuambia Mtandao Huu Kuwa Katika Mwaka Huu Matamasha Hayo Yatafanyika Kila Wilaya za Mkoa wa Njombe Ambapo Wasanii Mbalimbali Wanapata Fursa Ya Kujitangaza Vipaji Vyao Ikiwa ni pamoja na Kujitangaza Kupitia Kituo Hicho cha Radio.
Bwana Eugen Ameeleza Kuwa Lengo la Matamasha Hayo Katika Kipindi cha Mwaka Huu ni Kutokomeza Maambukizi ya UKIMWI Katika Mkoa wa Njombe Pamoja na Kuutangaza Mkoa Huo na Wasanii Wake.
Aidha Amesema Kuwa Kupitia Wasanii Hao Ambao Licha ya Kujitangaza Kwa Kuonesha Vipaji Vyao Majukwani Lakini Pia Watatumia Fursa Hiyo Kutoa Jumbe Mbalimbali Juu ya Ugonjwa wa UKIMWI Pamoja na Kuutangaza Mkoa Wa Njombe Ambao Bado Unachangamoto Nyingi.
Katika Hatua Nyingine Ametoa Fursa kwa Wafanyabiashara Mbalimbali Mkoani Njombe Kujitokeza Kutangaza Biashara Zao Kwa Kudhamini Matamasha hayo kwa Gharama ya Shilingi Laki Mbili kwa kila Tamasha Kupitia Kituo cha Radio Uplands Radio.
Amesema Kuwa Matamasha Hayo Yataanza Kufanyika Kuanzia Tarehe ya 22 Mwezi huu wa Machi Hadi Mwezi Julai Mwaka Huu Kwa Kuhitimisha Katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Njombe.