CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA MKOA WA NJOMBE[NJORECU] KIMEANZA UPYA BAADA YA KUSINZIA KWA KIPINDI SASA
Mgeni Rasmi Toka Mkoani Iringa Bwana John Kiteve Ambaye ni Mrajisi Msaidizi Wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Iringa Akiwasili Katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo Mjini Njombe Kwa ajili ya mkutano mkuu ![]()
Mwenyekiti wa Chama Hicho cha Ushirika Bwana Cremence Maleccela
Mrajisi Msaidizi Mkoa wa Iringa Bwana John Kiteve
Picha ya Pamoja Ya Wanachama wa Chama Hicho Baada ya Kumalizika Kwa Mkutano Mkuu Hapo Jana Njombe.
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Hapa Nchini Dokta Audax Mtabanziba Amewaagiza Viongozi wa Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Njombe[NJORECU]Kuhakikisha Wanatoa Ajira Kwa Watu Wenye Sifa Katika Ushirika Huo Ili Kuukuza na Kuuendeleza Kutokana na Uchanga Wake Baada ya Kusinzia Kwa Kipindi Kirefu.
Chama Hicho Cha Ushirika Kimeoneka Kusinzia Kwa Miaka Mingi Sasa Ikiwa Hapo Awali Kiliitwa NJOLUMA na Mara Baada ya Kubadilisha Jina Kuwa NJORECU Kwa Muunganisho wa Vyama Vya Wilaya Zote za Mkoa wa Njombe Kimeamsha Matumaini Ya Kuanza Upya Mkoani Hapa.
Akitoa Agizo Hilo Mrajisi Msaidizi Mkoa wa Iringa Bwana John Kiteve Kwa Niaba Ya Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Taifa,Amesema Kwa Kuwa Ushirika Huo Unaanza Tena ni Vyema Viongozi Wakahakikisha Wanatoa Ajira Kwa Watumishi Sahihi Badala ya Kutoa Ajira Kwa Upendeleo,Undugu na
Hata Kwa Rushwa Kwani Kufanya Hivyo Kutasababisha Kufifisha Matumaini Ya Chama Hicho Kwa Awamu Nyingne.
Pamoja na Mambo Mengine Bwana Kiteve Amewaagiza Viongozi Hao Kuhakikisha Wanatoa Taarifa za Maendeleo ya Chama Chao Kila Inapo Bidii Ili Kuondoa Hofu Kwa Wanachama Ambao Ndio Wahusika Wakuu wa Chama Hicho.
Akizungumza Mara Baada ya Kuhitimisha Mkutano Huo Mkuu wa Mwaka Uliofanyika Jana Katika Chuo cha Maendeleo Mjini Njombe Mwenyekiti wa Chama Hicho cha Ushirika Bwana Cremence Maleccela Amewahakikishia Wanachama Hao Kuwa Kwa Kuwa Wameamua Ushirika Huo Uanze Basi ni Lazima Ausimamie Vizuri Uweze Kwenda Mbele.
Bwana Maccela Amesema Tayari Wameshapita Katika Maeneo Mbalimbali Kwenye Vyama Vya Ushirika Mkoani Njombe na Kuhamasisha Suala la Wakulima Kuona Umuhimu wa Kutumia Vyama Vya Ushirika Kutokana na Hali Soko Lilivyo Kwa Sasa.
Jumla ya Vyama Vya Ushirika 59 Katika Wilaya Zote za Mkoa wa Njombe Vimekuwa Wanachama wa Chama cha Ushirika Mkoa wa Njombe NJORECU,Ushirika Uliokabidhiwa Rasmi Cheti Chake Hapo Jana Baada ya Kubadilishwa Kwa NJOLUMA.