Na James Festo Njombe
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Esterina Kilasi Jana Ametolea Ushahidi Wake Mbele ya
Mahakama ya Wilaya ya Njombe Dhidi ya Kesi ya Manunuzi Hewa wa Magurudumu Matano na Betri
Mbili za Gari Vyoti Vikiwa na Thamani ya Shilingi Milioni 14 Inayomkabili Aliyekuwa Katibu Tawala
Wilaya ya Njombe Evegray Keiya.
Akitoa Ushahidi Wake Mahakamani Hapo , Mkuu Huyo wa Wilaya ya Wanging'ombe Ameiambia
Mahakama Kuwa Ofisi Yake Pamoja na Aliyekuwa Akikaimu Ofisi ya Katibu Tawala Wilaya ya
Wanging'ombe Waliagiziwa Matairi Matano Aina ya Gunrub Kwa Ajili ya Gari Yake Lakini
Hakuwahi Kuyaona Magurudumu Hayo Katika Ofisi Yake .
Akitoa Ushahidi Mahakamani Hapo Shahidi Namba Mbili Ambaye ni Afisa Manunuzi wa Mkoa wa
Njombe Gaitan Malio Lugenge Ameiambai Mahakama Kuwa Alipokea Taarifa ya Ununuzi wa
Magurudumu Matano na Betri Mbili Aina ya N70 na Kusema Kuwa Betri Moja Liliwekwa Kwenye
Gari Lenye Namaba za Usajili STJ 6821 ya Katibu Tawala Mkoa wa Njombe .
Akiendelae Kutoa Ushahidi Mahakamani Hapo Shahidi Namba Mbili Gaitan Malio Lugenge
Ameieleza Mahakamani Hapo Kuwa Magurudumu Waliyoyapokea Yalikuwa Tofauti na Yale
Yaliyoagizwa Yanunuliwe Kwani Magurudumu Waliyoyapokea Yalikuwa ni Aina Ya Bridgestoni
Badala ya Gunrub.
Kwa Upande Wao Washtakaiwa Wakitetewa na Wakili Wao Hawakutakiwa Kujibu Chochote
Mara Baada Kusikiliza Utetezi wa Upande wa Mashtaka Hakimu wa Mahakama Hiyo John Kapokolo
Ameahirisha Kesi Hiyo Hadi Machi Tano Mwaka Huu Itakapo Sikilizwa Tena Mahakamani Hapo na
Washitakiwa Wameachiwa Kwa Dhamana.
Katika  Kesi Nyingine Afisa Tawala Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Njombe Anna Wiketye
Mwenye Umri wa Miaka 33 Mkazi wa Mtaa wa Bomani Mjini Njombe  Amefikishwa Mahakamani
Hapo Kujibu Shtaka Linalo Mkabili La Kutoa Ushahidi Wa Uongo Kinyume Na Kifungu Cha Sheria
Namba 102 Sura Ya Kwanza Na Kifungu Namba 104 Sura Ya 16 Cha Sheria Za Makosa ya JinaiÂ
Kanuni Ya Adhabu Katika Kesi Inayomkabili Aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Njombe.
Akisoma Hati Ya Mashtaka Mahakamani Hapo Mwendesha Mashtaka Wa Serikali Bwana RizikiÂ
Matitu Amesema Kuwa Novemba 18 Mwaka Jana Mshtakiwa Alifikishwa Mahakamani Hapo Ili
kutolea Ushahidi Wa Kesi Ya Bw.Bori Salunge Ally, Evegray Keiya na Bw Ibrahim Konga  na kutoa
Ushahidi wa Uongo ulioufanya Upande Wa Mashitaka Kumuondoa Katika Orodha ya MashahidiÂ
Kwenye Kesi ya Matumizi Mabaya ya Ofisi na Kusababisha Hasara ya Shilingi Milioni Mbili zaÂ
Wilaya Hiyo.
Kwa Upande Wake Mshitakiwa Huyo Akijibu Mashtaka Yanayomkabili Mahakamani Hapo Amesema
Alikubali Kutoa Maelezo Kwa Maofisa wa Takukuru na Kwamba Ushahidi Huo Aliutoa Kutokana
na Mazingira Aliyokuwa Nayo Wakati Akihojiwa Katika Ofisi Hizo na Haukuwa Hiari Yake.
Hata Hivyo Hakimu wa Mahakama Hiyo Ameahirisha Kesi Hiyo Hadi Machi Tano Mwaka Huu na
Mshitakiwa Yuko Nje Kwa Dhamana.Â