ASASI YA KIBENA WOMEN ASSOCIATION YAFANYA HAFLA YA KUFUNGA MWAKA NA WATOTO YATIMA.
Picha ya Pamoja na Watoto Yatima Wanaolelewa na Asasi ya Kibena Women Association![]()
Uongozi wa Asasi Hiyo
Mkurugenzi wa Mtandao huu Bwana Gabriel Kilamlya Akizungumza Jambo Wakati wa Hafla Hiyo.
Mgeni Rasami wa Hafla hiyo ya Watoto Yatima Bi.Lilian Nyemele Ambaye ni Afisa Tarafa ya Njombe Mjini Akihutubia JamiiIliyokleti na
Watoto Hao Mkurugenzi wa KIBENA WOMEN ASSOCIATION Bi. Betty Liduke Akieleza hali ya malezi ya watoto hao
Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Mji wa Njombe Akizungumza na Watoto hao.
Mgeni rasmi akiendelea kugawa zawadi kwa watoto hao
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Serikali Imelaani Kitendo cha Baadhi ya Wazazi Kuwashawishi Wanafunzi Wasifanye Vizuri Katika Masomo Yao Kwa Kile cha Kugoma Kuendelea Kuwalipia Karo za Shule.
Agizo Hilo Limetolewa na Afisa Tarafa Ya Njombe Mjini Bi.Lilian Nyemele Wakati wa Hafla ya Watoto Wanaoishi katika mazingira hatarishi na Yatima Iliyofanyika kibena Mjini Njombe
Bi.Nyemele Amesema Kuwa Kitendo Cha Baadhi ya Wazazi Kudiriki Kuwashawishi Wanafunzi Kuto fanya vizuri katika masomo yao ni kuwaharibia Maisha yao ya Baadaye.
Pamoja na Mambo Mengine Amewataka Wadau Mbalimbali Yakiwemo Mashirika Yasiyo Yakiserikali na Ya Kiserikali Kutambua Adha Wanayoipata Wanafunzi Ambao ni Yatima Katika Maeneo Yao.
Hata Hivyo Ameeleza Kuwa Kumekuwa na Changamoto Mbalimbali Wanazokumbana nazo Katika Maisha yao ya Kila Siku Ambapo Jamii Nzima Kiujumla Inawajibu Wa Kuhakikisha Watoto Wanapata Elimu bora.
Pia Amewataka wanafunzi Hao Hususani wa Kike kuachana na Tabia ya Kujiingiza katika makundi hatarishi yatakayowapelekea kupata mimba wakati wa masomo pamoja na Utumiaji wa Madawa ya Kulevya.
Awali Akimkaribisha Mgeni Rasmi Katika Hafla Hiyo Iliyoandaliwa na Shirika Lisilo la Kiserikali la KIBENA WOMEN ASSOCIATION Mkurugenzi wa Shirika Hilo Bi.Betty Liduke Amesema Kuwa Shirika Hilo Limechukua Jukumu la Kuwasaidia watoto Hao Ambao Wamekuwa wakishindwa Kupata Elimu Bora Baada ya Wazazi Wao Kufariki.
Bi.Liduke Ameeleza Kuwa Pamoja na Kazi Hiyo Ambayo Wamekuwa Wakiifanya Lakini Wakumbana na Changamoto mbalimbali Ikiwemo Baadhi ya Wanafunzi Kugoma Kuendelea na Masomo Bila Sababu za Msingi Ilihali Gharama zimeshalipwa.
Aidha Ameongeza Kuwa Walezi wa Watoto hao Wamekuwa wakiwaachia Majukumu yote Wakidhani Shirika Hilo Linafedha Nyingi Kitu ambacho Kimekuwa kikiwapa Wakati Mgumu Katika Kuendelea Kuwasaidia Watoto Hao.
..........................................................................................................