SERIKALI YA MKOA WA IRINGA YAMLILIA MWANAFUNZI ALIYEFUTIWA MATOKEO KWA UDANGANYIFu.![]()
katibu wa kikao cha uteuzi wa wanafunzi Bi Wamoja Ayub ambae ni katibu tawala mkoa akifunga kikao cha uteuzi ,kulia kwake ni ofisa elimu msingi mkoa Bw Joseph Mwinyikambi
...........................................................................................................................
Akizungumza leo katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo wakati wa kikao cha uchaguzi wa wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu , katibu wa kikao hicho Wamoja Ayub ambae ni katibu tawala wa mkoa wa Iringa alisema kuwa mkoa wa Iringa unajivunia kuendelea kushika nafasi ya tatu kwa miaka miwili mfululizo sasa.
SERIKALI mkoani Iringa imepongeza ufaulu mzuri wa wanafunzi wa darasa la saba mwaka huu 2013 kuwa ni ufaulu mzuri uliouwezesha mkoa wa Iringa kushika nafasi ya tatu kitaifa kati ya mikoa 25 Tanzania bara ,huku ukimlilia mwanafunzi mmoja wa shule ya Msingi Mabaoni wilayani Mufindi ambae amefutiwa matokeo yake kutokana na udanganyifu .
Huku wabunge wawili kati ya 9 waliohudhurika kikao hicho akiwemo Mbunge wa jimbo la Mufindi kusini Mendrady Kigola na mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazin Bw Mahamudu Mgimwa wakiipongeza wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kutokana na utendaji kazi mzuri kwa kuwezesha watahiniwa wanafunzi 14,956 wakiwemo wavulana 7,042 na wasichana 7,914 sawa na asilimia 65.25 mkoani Iringa kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2014.
Hata hivyo alisema kuwa lengo la mkoa wa Iringa kwa mwakani kuongeza jitihada zaidi ili ikiwezekana kuushusha mkoa wa Dar es Salaam katika nafasi ya Kwanza na Kilimanjaro katika nafasi ya pili na mkoa wa Iringa kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya darasa la saba mwakani 2014
Kuhusu udanganyifu katika mitihani alisema kuwa suala hilo lina madhara makubwa kitaifa na kuwa suala hilo limekuwa likipigiwa kelele na serikali kutokana na athari zake kuwa kubwa kwa wanafunzi wanaohusika na udanganyifu kama ilivyo kwa mwanafunzi Atupelye Mligo wa shule ya Msingi Mabaoni Mufindi aliyefutiwa matokeo yake .
Pia alisema kwa mwalimu aliyehusika na tukio hilo la udanganyifu mwalimu Edwin Ambokele wa shule ya msingi Makungu kwa sasa kesi yake ipo mahakamani akisubiri mkono wa sheria unasemaje katika suala hilo.
Bi Wamoja alisema kuwa jambo hilo ni la aibu kwa mkoa wa Iringa na Taifa kwa ujumla hivyo aliwaonya walimu na maofisa elimu mkoani Iringa kuendelea kukemea suala hilo ili lisije tokea tena katika mkoa wa Iringa .
Aidha aliwataka wakurugenzi na wakuu wa wilaya kusimamia ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuwezesha wanafunzi waliochaguliwa kuanza masomo kwa wakati hasa akisisitiza zaidi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ambayo ina idadi kubwa ya wanafunzi waliochaguliwa kuliko idadi ya vyumba vya madarasa kuhakikisha wanakamilisha mapema ujenzi wa shule ya sekondari Nduli ili wanafunzi waliopangwa katika shule hiyo kuanza masomo kwa wakati.
Akisisitiza juu ya malengo ya matokeo makubwa sasa katika sekta ya elimu alisema kuwa Manispaa ya Iringa inapaswa kufikia asilimia 90 kwa mwaka 2014 wakati Halmashauri ya Iringa ina lengo la kufikia asilimia 76 wakati Kilolo ni asilimia 77 huku Hlamshauri ya Mufindi inalengo la kufikia asilimia 79 kuwa hayo ni malengo yaliyopo katika utekelezaji wa matokeo makubwa sasa katika mkoa
Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wameeleza kusikitishwa kwao na hatua ya wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi kushindwa kushiriki katika kikao hicho nyeti na kuwaacha wabunge wawili pekee wa jimbo la Mufindi kusini na Kaskazini kushiriki kikao hicho huku wengine wote wakishindwa kutokea .
Wabunge wanaounda mkoa wa Iringa ni Prof Peter Msolla Kilolo( CCM) mchungaji Peter Msigwa -Chadema Iringa mjini, Dr Wiliam Mgimwa - Kalenga (CCM)Mahamundu Mgimwa - Mufindi kaskazin ( CCM)Mendrady Kigola - Mufindi kusini (CCM) Wiliam Lukuvi - Isimani (CCM ) ,Ritta kabati - Viti maalum (CCM)-Lediana Mafulu - Viti maalum (CCM) na Chiku Abwao -Viti Maalum (Chadema)
Mbunge wa Kalenga Dr Mgimwa yawezekana ameshindwa kufika kutokana na sababu ya kiafya inayomsumbua na yupo nje ya nchi wakati mbunge wa Ismani Wiliam Lukuvi pia yawezekana ameshindwa kufika kutokana na majukumu ya nafasi yake ya uwaziri.
Mbunge wa Kalenga Dr Mgimwa yawezekana ameshindwa kufika kutokana na sababu ya kiafya inayomsumbua na yupo nje ya nchi wakati mbunge wa Ismani Wiliam Lukuvi pia yawezekana ameshindwa kufika kutokana na majukumu ya nafasi yake ya uwaziri.
Akitangaza matokeo hayo kwa mkoa wa Iringa afisa elimu msingi Bw Joseph Mwinyikambi alisema kuwa jumla ya wanafunzi waliofanya mtihani huo mwaka huu ni 14956 sawa na asilimia 65.2 na waliofaulu ni 14,956 sawa na asilimia 65.2 huku wanafunzi 7966 wakiwemo wasichana 4378 na wavulana 3588 sawa na asilimia 34.8 wakifeli katika mtihani huo
Huku wanafunzi 226 wakishindwa kufanya mtihani huo kutokana na sababu mbali mbali idadi yake kwenye mabano ,utoro (196),vifo (12), ugonjwa (13) na mimba (5).
Wakati Halmashauri ya Manispaa ya Iringa yenye idadi ya shule za msingi 47 ikiongoza kwa kushika nafasi ya kwanza kwa miaka miwili mfululizo sasa ikifuatiwa na Halmashauri ya Iringa yenye shule 138 kwa kushika nafasi ya pili wakati Kilolo yenye shule 101 ikishika nafasi ya tatu na Mufindi yenye shule 163 ikishika nafasi ya mwisho katika matokeo hayo.
kwa Hisani ya FG Blog