Mshereheshaji wa Mahafali Hiyo Bwana Prosper Daud Mfugale Ambaye ni Mwanahabari wa Kituo cha Redio Mjini Njombe Akifanya Yake.
Wahitimu wa Fani Mbalimbali Katika Chuo cha Eckross Kilichopo Mjini Njombe
Prosper Mfugale na Steven Ngole Njombe
Wazazi Mkoani Njombe Wametakiwa Kuwaendeleza Watoto Wao Kitaaluma Ikiwa ni Pamoja na Kuwapatia Mafunzo ya Fani Mbalimbali Zinazotolewa na Taasisi na Chuo Vilivyopo Mkoani Njombe Jambo Ambalo Litasaidia Kupunguza Tatizo la Ajira Miongomni Mwa Vijana Mkoani Hapa.
Akizungumza Kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Benki ya NJOCOBA Wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Cha Utalii na Uandishi wa Habari Cha Eckros Njombe,Mwakilishi wa Mkurugenzi Bw Mfikwa Amesema Kuwa Vijana Wanaweza Kuondokana na Tatizo la Ajira Endapo Wataendelezwa Kitaaluma na Hivyo Kuwataka Wazazi Kutokata Tamaa Dhidi ya Vijana Hao.
AmesemaPamoja na Mambo Mengine Uongozi wa Chuo Unatakiwa Kutatua Baadhi ya Changamoto Zinazokikabili Chuo Hicho Ili Kuhakikisha Inaboresha Hali ya Taaluma na Kiwango Cha Elimu Inayotolewa Chuoni Hapo Jmabo Litakalosaidia Kuwa na Wahitimu Wenye Uwezo Kitaaluma na Kufanya Kazi Kwa
Ubora.
Awali Akisoma Risala Kwa Niaba ya Wahitimu Mmoja wa Wahitimu Katika Fani ya Uandishi wa Habari Ester Pascal Ameuomba Uongozi wa Chuo Kutatua Baadhi ya Changamoto Zinazokikabili Chuo Hicho Ikiwemo Upungufu wa Vifa Hasa Kwa Fani za Uandishi wa Habari na Ufundi Mitambo.
Katika Mahafali Hayo UJumla ya Wahitimu 72 Walitunukiwa Vyeti Vya Kuhitimu Fani Mbalimbali Ikiwemo Utalii,Uhudumu wa Hoteli,Katibu Muhtasi,Ufundi Mitambo na Uandishi wa Habari.