WANANCHI WA KIJIJI CHA ITULAHUMBA WAAHIRISHA SHUGHULI ZAO KWA AJILI YA KUMNG'OA MWENYEKI WA KIJIJI CHAO.![]()
AFISA TAARAFA YA MDANDU BENSON WANDERAGE AKIWA KWENYE MKUTANO WA HADHA AMBAO ULIKUSUDIA KUWAKATAA VIONGOZI WA KIJIJI AMBAO NI MWENYEKITI NA MTENDAJI ALIYEHAMISHIWA KIJIJINI HAPOHUyU NI MWENYEKITI ALIYEKAIMISHWA BWANA SHAIBU MAHEGELE BAADA YA WANANCHI KUMFUKUZA MWENYEKITI WA ZAMANI BWANA HOSEA MPOSOLA
HUYU NI MWENYEKITI WA KIJIJI BWANA HOSEA MPOSOLA ALIYEFUKUZWA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA ITULAHUMBA WAKISEMA HAWANA IMANI NAE
Na Michael Ngilangwa
Hatimae sakata la wananchi wa kijiji cha Itulahumba la kuwakataa viongozi
limeingia sura mpya baada ya wananchi hao kumufukuza mwenyekiti wao na
kumuchagua mwenyekiti wa muda huku wakimuomba mkurugenzi kumuondoa afisa
mtendaji ambae amepelekwa hivi karibuni kusimamia maendeleo ya kijiji hicho.
Wakiongea mbele ya viongozi wa kata na taarafa ya Mdandu wananchi hao
wameelezea sababu za kumkataa mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Hosea Mposola
kwa kuruhusu afisa mtendaji aliyekuwepo bwana Method Mligo kuhamia kijiji cha
Itambo bila kusoma hesabu za mapato na matumizi,kuruhusu afisa mtendaji mpya
kuhamia katika kijiji hicho pasipo wananchi kufahamishwa uwepo wake jambo
lililopelekea wananchi kutokuwa na imani na mwenyekiti huyo.
Kuhusu afisa mtendaji aliehamishiwa katika kijiji hicho akitokea kijiji cha Itambo
bwana Batista Msemwa wananchi hao wamesema kuwa hawamuhitaji
mtendaji huyo kutokana na wananchi wa kijiji cha Itambo kumkataa kutokana na kutuhumiwa kuhusika na ubadhilifu wa mali za kijiji cha Itambo na kwamba serikali imekuwa na tabia ya kuwahamishia vijiji vingine watumishi wanaotuhumiwa na ubadhilifu wa mali za wananchi ili waendelee na ufujaji wa mali za wananchi.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara afisa taarafa ya Mdandu bwana Benson
Wanderage amesema kufuatia kuteuliwa kwa mwenyekiti wa muda wananchi
wanatakiwa kuonesha ushirikiano katika kutekeleza miradi ya kijiji hicho huku
akisema kuwa serikali ya kata itakwenda kumuagiza afisa mtendaji aliyehamishwa
arudi kijijini hapo ili asome taarifa ya hesabu za mapato za matumizi.
Diwani wa kata ya Mdandu bi Anna Upendo Gombela amesema amewapongeza wananchi kwa mahudhurio ya wananchi hao na kwamba lengo la kuwakutanisha wananchi hao ni kutatua mgogoro uliokuwepo baina ya viongozi na wananchi wa kutokuwa na imani na uongozi wa kijiji akiwemo mwenyekiti huku akisema wajumbe wa serikali ya kijiji wameridhia kufanya uteuzi wa mwenyekiti wa muda ambae anakubalika na wananchi wote.
Afisa mtendaji wa kata ya Mdandu bwana Timoth Fute amesema kuwa ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe tayari imechukua hatua za kumuandikia barua yakwenda kusoma hesabu za mapato na matumizi ya kijiji cha Itulahumba mtendaji huyo pindi atakapo pona kwani kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Kibena ambapo ameahidi kumsimamia ili kuhakikisha anakwenda kusoma taarifa za mapato na matumizi ya kijiji hicho ndipo aweze kahama.