Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

KARIBU UTANGAZE NA MTANDAO HUU KWA BEI NAFUU, Fursa nzuri kwa Mfanyabiashara wa Mkoa wa Njombe.

$
0
0

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI ATEMBELEA KARAKANA YA RELI MJINI MOROGORO.


Mafundi wa kampuni ya SMH/Rail ya nchini Malaysia wakiendelea na kazi ya kuunda upya moja wapo ya vichwa vya treni ambavyo vinaundwa kwenye karakana ya Reli mkoani Morogoro. Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi alitembelea karakana hiyo kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Vichwa hivyo ambapo wamemuahidi kichwa cha kwanza kitakabidhiwa kwa Serikali mwanzoni mwa mwezi Disemba 2013.

Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akiongea na vibarua walioajiriwa na kampuni ya SMH/Rail kutoka nchini Malaysia, asubuhi alipofanya ziara kwenye karakana ya Reli mkoani Morogoro kuangalia maendeleo ya uundwaji upya wa Vichwa vya Treni vya Shirika la Reli Tanzania(TRL). Naibu Waziri huyo ameuagiza uongozi wa kampuni hiyo kuhakikisha kuwa vibarua hao wanapewa mikataba kama watafanya kazi zaidi ya miezi mitatu kama sheria za kazi zinavyowataka.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akioyeshwa mpango kazi wa kampuni ya SMH/Rail na Mhandisi wa Kampuni hiyo, Eng. Mohd Hisham(Kulia kwa Naibu Waziri) ambayo inaunda upya vichwa vya treni katika karakana ya Reli Mkoani Morogoro. Naibu Waziri ametembelea karakana hiyo leo Asubuhi kuangalia maendeleo ya undwaji upya wa vichwa vya treni ambavyo viko kwenye mpango wa matokeo makubwa sasa kwenye sekta ya Uchukuzi.

Naibu Waziri wa Uchukuzi akiongea na Naibu Mtendaji Mkuu, Uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Paschal Mafikiri (wa kwanza kushoto), wakati alipotembelea Karakana ya Reli Mkoani Morogoro, leo asubuhi kuangalia maendeleo ya undwaji upya wa vichwa vya treni. Kichwa cha kwanza kinategemea kukamilika mwanzoni mwa Mwezi wa Disemba 2013.

CREDIT michuziblog

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles