Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276
↧

RC NJOMBE AAGIZA KUVUNJWA KWA MAKUNDI KWA MADIWANI WILAYA YA WANGING'OMBE .

$
0
0
.Ni wakati wa Kikao cha kwanza cha baraza la madiwani Katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe.
 

 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi Akiwasili Kwenye Kikao Cha Kwanza cha Baraza la Madiwani  Katika Ukumbi wa Primium Power Point Uliopo Kwenye Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging'ombe Igwachanya.

 Baadhi ya Madiwani wa Kata Mbalimbali za Wilaya ya Wanging'ombe Wakiwa Kwenye Kikao cha Kwanza Cha Baraza la Madiwani Leo.,Wamekosa Yunifomu Kutokana na Kwamba Kikao Hicho ni Cha Kwanza.

 Pichani ni Mkurugenzi wa Halmashauri Mpya ya Wilaya ya Wanging'ombe Bi.Lucy Msofe.
 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi Akiagiza Kuvunja Makundi Kwa Madiwani Katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe.
 Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi Mhandisi Gerson Lwenge Akikemea Tabia ya Madiwani Kutoa  Nje Siri za Makubaliano Yanayofikiwa Kwenye Vikao na Kuleta Mkanganyiko kwa Jamii.
 Mkuu wa Wilaya ya Makete Bi.Josephine Matiro Aliyemkaimu Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Esterina Kilasi Akizungumza Kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Wilayani Wanging'ombe Leo.
 Baadhi ya Wakuu wa Idara na Wataalamu Katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Ambao Kwa Asilimia 99.9 Wamekaimu Vyeo Hivyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Bwana Antony Emmanuel Mahwata Akifunga Kikao cha Kwanza cha Baraza la Madiwani  Leo Huko Igwachanya.

Na   Gabriel  Kilamlya Wanging'ombe.

Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi Amewaagiza Madiwani wa Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Kuvunja Makundi Yaliyokuwepo Baina Yao Yaliyotokana na Uchaguzi wa Wenyeviti na Kamati Mbalimbali Katika Halmashauri Hiyo.

Agizo Hilo Amelitoa Leo Kwenye Kikao Cha Kwanza Cha Baraza la Madiwani Katika Halmashauri Hiyo  Kufuatia Kuwepo Kwa Makundi Yanayoweza Kuwagawa Wananchi Katika Shughuli za Kimaendeleo Ilihali Wote ni Madiwani wa

Wilaya Moja.

Pamoja na Mambo Mengine Captain Mstaafu Msangi Ameitaka Halmashauri Ya Wilaya ya Wanging'ombe Kuweka Bajeti ya Kilimo Cha Zao la Karanga Kutokana na Zao Hilo Kustawi Vizuri Wilayani Humo na Hivyo Zao Hilo Liwe Tegemeo Kama zao La Kuinua Uchumi Kwa Wananchi wa Wilaya Hiyo.

Wakizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Mara Baada ya Kikao Hicho Baadhi ya Madiwani Hao Wameiomba Serikali Kuwaongezea Magari Katika Halmashauri Hiyo Ambayo ni  Mpya Ili Kuharakisha Huduma Kwa Wananchi.

Hata Hivyo Wamesema Kuwa Wataalamu Katika Halmashauri Hiyo Wamekuwa Wakishindwa Kufanya Kazi Zao Kwa Wakati Kutokana na Uhaba Mkubwa Wa Vyombo Vya Usafiri Kwenye Halmashauri Hiyo.

Mhandisi Gerson Lwenge ni Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi na Naibu Waziri wa Ujenzi Ambaye Amelaani Tabia ya Baadhi ya Viongozi Wakiwemo Madiwani Kutoa Siri za Makubaliano Ya Vikao na Kuyafikisha Kwa Wananchi.

Kwa Mara Ya Kwanza Halmashauri Ya Wilaya ya Wanging'ombe Imefanya Kikao cha Kwanza Cha Baraza la Madiwani,Halmashauri Iliyoonekana Kuwa na Changamoto Nyingi Kutokana na Upya Wake.
...........................................................................................................................
↧

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Latest Images

Trending Articles