Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 1

$
0
0
NI VIGEZO GANI HUTUMIKA KATIKA KUSHINDA TUZO YA USAFI WA MAZINGIRA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE?

Hili ni dampo Lililopo Nyuma ya Stendi Kuu ya Mabasi Mjini Sehemu Ambayo Biashara za Nguo na Vyakula zinafanyika.

Dampo Hili Mara kwa Mara Linaonekana Kujaa na Kuhatarisha Afya za Wakazi wa Maeneo hayo Kutokana na kushamiri kwa Uchafu kitu kinachopelekea Dampo hilo Kujaa hadi Taka Kumwagikia Pembeni  kama Linavyoonekana Hapo.

Leo Septemba 10 2013 mtandao huu Umetembelea Dampo Hili na Kushuhudia Hali Hii,na Njia Karibu Inaziba.

Mbali na Dampo Hili Kuwa Jirani na Mama Lishe wanaopika Vyakula na Wafanyabiashara wa Nguo za Mitumba kushinda Humo Ndani Lakini Pia Taka Hizo Zipo jirani kabisa na Kituo cha Afya Cha Njombe Mjini Ambako Hata Afisa Afya Yupo Jirani na Dampo Hili.

Halmashauri ya Mji wa Njombe ndio yenye Mamlaka ya kuhakikisha Inafanya Usafi Katika Eneo hili kwa Kuwa Huchukua Ushuru kwa Wafanyabiashara hao.

Wakala anayefanya kazi Hii Awali Alikuwa Akilalamikia Kuto lipwa Fedha yake sasa haijulikani kama Kazila au Kasusia kwa Muda.

Lakini Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Mji wa Njombe Imekuwa Ikishinda Mashindano ya Usafi wa Mazingira Karibu Kila Mwaka,Swali langu'.je ni
vigezo gani Hutumika?

Au Halmashauri hii hushinda kwa kuangalia usoni mwa Barabara tu ambamo usafi huonekana ukifanywa?

Salamu za Mjomba zilitembea sana lakini mwisho wa Siku zika ishia hapa"SAFARI IMENISHINDA SASA NARUDI KWETU"

Haina maana Kuwa Mjomba Kazi Ili Mshinda lakini aliona Kuwa Anaweza Kutumia Nguvu kubwa hadi kujisababishia Matatizo kwa kupiga Kelele Bila Mafanikio.

Hizi ni salamu za mtandao huu wa www.gabrielkilamlya.blogspot.com.

Hata wewe pia waweza Kutoa Ushauri Pia kwa Halmashauri yetu,Labda haina Bajeti ya Usafi katika eneo hili au, Inampango wa Kuwasusia wakazi wa Maeneo haya.

Lakini hata Wafanyabiashara wa Nguo katika eneo Hili waliambiwa wahame,huenda akufukuzae hakwambii toka.!!!!!!!!!

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles