Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 4

$
0
0

DEREVA BODA BODA AUAWA  KINYAMA IRINGA


Edger Lalika akiwa  wodini kabla ya  kufariki dunia.................................................................................
 _______________________________________________________
 Francis Godwin na  kayanda manyanya,Iringa 

Zikiwa  zimepita  siku  chache  toka  mmoja kati ya madereva boda boda mjini Iringa kutekwa kisha  kujeruhiwa vibaya kablaya kuporwa  pikipiki  yake ,unyama huo dhidi ya madereva  boda boda  umeendelea kutikisa mji wa Iringa baada Kijana mmoja mkazi wa kihodombi kutekwa kisha kuuwawa kinyama.
Tukio hilo la kinyama  limetokea  usiku  wa  leo baada ya kijana  huyo aliyetambulika kwa  jina la Edger Lalika kukutwa ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani .
Mashuhuda  wa  tukio hilo  wameueleza mtandao  huu wa matukio daima .com kuwa tukio la kuuwawa  kwa  dereva  boda  boda  huyo liletokea eneo la 
Tosamaganga wilaya ya Iringa mkoani Iringa.
Hata  hivyo kijana  huyo anayekadiliwa  kuwa na umri wa miaka 20,ameuwa akiwa anafanya shughuli zake za bodaboda baada  ya  kukodiwa na mteja  wake huyo ambae aliamua  kuitoa roho yake kabla ya kumpokonya boda boda.
Kutokana na tukio  hilo  baadhi ya madereva bodaboda wamelaani vikali kitendo hicho na kuwataka madereva bodaboda wengine kuungana na kushirikiana na jeshi la polisi kufichua vitendo hivyo  vya utekaji na mauwaji  dhidi ya madereva  boda boda.
 Mazishi ya kijana huyo yanafanyika leo katika makaburi ya mlolo Iringa mjini

Jeshi la  polisi mkoa  wa Iringa  limethibitisha  kutokea kwa mauwaji  hayo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles