Haya ni Badhi ya maeneo yanayo Limwa na wananchi wa Mtaa wa Maheve Karibu na Vyanzo vya Maji Mjini Njombe.
Na Prosper Mfugale Njombe
Serikali Wilayani Njombe Imesema Itaendelea Kuwachukulia Hatua za Kisheria Wananchi Ambao Wanaendelea na Shughuli za Kilimo Kwenye Maeneo ya Vyanzo Vya Maji na Kusababisha Uharibifu wa Mazingira.
Kauli Hiyo ya Serikali Imekuja Kufuatia Malalamiko ya Baadhi ya Wananchi na Wadau Kudai Kuwa Sheria ya Utunzaji wa Vyanzo Vya Maji Inayokataa Kuendesha Shughuli za Kiuchumi Ikiwemo Kilimo Kwa Umbali Mita Sitini Kutoka Chanzo cha Maji Kuwa Inapelekea Wananchi Hao Kukosa Mavuno ya Uhakika.
Akiongea na Kituo Hiki Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sara Dumba Amesema Zinahitajika Jitihada Zaidi Katika Utunzaji wa Mazingira Hasa Vyanzo Vya Maji Ili Kukabiliana na Tatizo la Ukame Linaloanza Kujitokeza Kufatia Wananchi Wengi Kuendesha Shughuli za Kiuchumi Kando ya Vyanzo Vya
Maji Pamoja na Kupanda Miti Ambayo Si Rafika na Vyanzo Hivyo.
Kwa Upande Wao Baadhi ya Wananchi na Wadau Hao Wamesema Uharibifu wa Mazingira Pamoja na Vyanzo Mbalimbali Vya Maji Inasababishwa na Baadhi ya Watu na Makampuni Yanayopanda Miti Ambayo Si Rafiki na Vyanzo Vya Maji.
Licha ya Kuwa Wilaya ya Njombe ni Miongoni Mwa Wilaya Zenye Vyanzo Vingi Vya Maji na Mvua za Kutosha Lakini Wilaya Hiyo Inakabiliwa na Tatizo la Upatikanaji wa Maji ya Uhakika Kwa Muda Mrefu .