MAKATIBU WA CCM WA WILAYA WALIOTEULIWA hawa hapa.
UTEUZI
Kikao cha Halmashauri Kuu pia kimeridhia, uteuzi wa Makatibu wateule wapya wa Jumuiya za CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuia ya Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).
Katika uteuzi huo mapendekezo hayo yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM na kuridhiwa na NEC, kwa upande wa UVCCM ameteuliwa aliyekuwa Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda na kwa upande wa Jumuia ya Wazazi ni Mjumbe wa NEC kutoka Pemba, Seif Shabani Mohamed, huku kwa upande wa UWT akiachwa Katibu Mkuu wa sasa, Amina Makilagi.
Mapunda atachukua nafasi iliyokuwa imneshikiwa na Martine Shigela ambaye ameongoza UVCCM kwa miaka mitano sasa, na Seif Shabani Mohammed kutoka Pemba akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Hamis Suleiman Dadi ambaye pia amekuwa katika wadhifa kwa miaka mitano sasa.
Pia, NEC imeridhia mapendekezo ya Kamati Kuu kwa ajili ya kuziba nafasi Makatibu wa CCM wa mikoa mitatu ya Morogoro, Kaskazini Pemba na Geita ambayo kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa imekuwa wazi kwa muda mrefu sasa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo.
Kufuatia mapendekezo hayo ya Kamati Kuu, ambayo yameridhiwa na NEC, walioteuliwa na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni Msaidizi Kitengo cha Uchaguzi, CCM Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Romuli Rojas John (Morogoro), aliyekuwa Katibu Katibu wa wilaya ya Mkinga, Kassim Mabrouk Mbarak (Kaskazini Pemba) na aliyekuwa Katibu wa CCM Igunga, Mary Maziku (Geita).
Kuhusu sakata la madiwani wa Bukoba mjini, CCM imesema suala hilo, linaendelea kushughulikiwa ambapo baada ya kikao hicho cha NEC, Kamati kuu iliendelea kukutana na viongozi wa wilaya ya Bukoba, Mwenyekiti wa CCM na Katibu wa wilaya hiyo.
Mapema kabla ya kikao cha NEC, Kamati Kuu ilikutana na Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba mjini na kuwahoji, wakati jana Kamati Kuu ilikutana na Mwenyekiti na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera.
Taarifa Rasmi ya CCM ya majina ya Makatibu wa Wilaya walioteuliwa na NEC
Ndugu Ashura Amanzi
Ndugu Rukia Saidi Mkindu
Ndugu Elias J. Mpanda
Ndugu Jonathan M. Mabihya
Ndugu Mulla Othman Zuberi
Ndugu Jumanne Kapinga
Ndugu Ali Haji Makame
Ndugu Jacob G. Makune
Ndugu Juma A. Mpeli
Ndugu Hawa Nanganjau
Ndugu Abdulrahman Shake
Ndugu Subira Mohamed Ameir
Ndugu Abdallah Shaban Kazwika
Ndugu Juma Bakari Nachembe
Ndugu Josephat Ndulango
Ndugu Rajab Uhonde
Ndugu Abeid Maila
Ndugu Mohamed Lawa
Ndugu Mariam Sangito Kaaya
Ndugu Bakar Lwasa Mfaume
Ndugu Julius Peter
Ndugu Jumanne Kitundu Mginga
Ndugu Mathias NyombiNdugu Mohamed Hassan Moyo