Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba.
Na Michael Ngilangwa Njombe.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Sara Dumba Amewataka Wachimbaji Wadogo wa Madini Wilayani Njombe Kuzingatia Taratibu za Kuomba Leseni Kwa Wakati Kabla ya Kuanza Shughuli za Uchimbaji Ili Kuhepusha Migogoro Inayotokana na Wachimbaji Wengi Kutozingatia Taratibu Zilizopo Katika Uchimbaji wa Madini.
Aidha Mkuu Huyo wa Wilaya Pia Amewataka Maafisa wa Madini Kuwasaidia Waombaji wa Leseni Kwa Uadilifu na Kwa Kuzingatia Maadili ya Utumishi wa Umma Jambo Ambalo Linapaswa Kutekelezwa na Maafisa Hao Ili Kupunguza Migogoro Hiyo.
Akisoma Taarifa ya Mgogoro wa Uchimbaji Madini Katika
Kijiji Cha Uliwa Wilayani Njombe,Mbele ya Makamishna wa Madini Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Amesema Kwa sasa Mgogoro Huo Tayari Umeshapatiwa Ufumbuzi Baada ya Pande Zote Kukutanishwa na Kufikia Muafaka Kuhusu Uchimbaji wa Madini Katika Kijiji Hicho.
Amesema Serikali Itaendelea Kusikiliza Kero za Wananchi na Kuhakikisha Inazipatia Ufumbuzi Kadiri Inavyowezekana Huku Akitoa Angalizo Kwa Viongozi wa Vyama Vya Siasa Kuwaeleza Ukweli Wananchi Kuhusu Mambo Yanayojitokeza Katika Maeneo Yao.
Kwa Upande wake Kamishna Msaidizi wa Utoaji wa lesseni za Madini Kanda ya Kusini John Nayopa Amewataka Watafiti na Waombaji wa Lesseni za Uchimbaji wa Madini Mkoani Njombe Kuhakikisha Wanazingatia Taratibu Zilizopo Ili Kuhepuka Migogoro ya Mara Kwa Mara.
............................................................................................................................