Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 4

$
0
0
APOTEZAMAISHAAKIFYATUA TOFALI MAHEVE NJOMBE 
Aangukiwa na kifusi
 Mwili wa Marehemu Ukiwa Umefunikwa mara baada ya Kufukuliwa kwenye Kifusi

Na Gabriel Kilamlya Njombe

Mtu Mmoja Juma Liduke Mkazi wa Makambako Mwenye Umri Kati ya Miaka 30-35  Amefariki Dunia Baada ya Kufukiwa na Kifusi Alicho kuwa Anafyatulia Tofali Leo Asubuhi.

Tukio Hilo Limetokea Katika Mtaa wa Maheve Eneo la Howadi Mjini Njombe Ambako Alikuwa Akifanya Shughuli za Kufyatua Tofali kama Kibarua Kwa Bwana Chesco Mwogofi.

Mashuhuda wa Tukio Hilo Ambao walikuwa wakifanya Kazi naye Wamesema Kuwa Walisikia Kelele mara Moja walipogeuka wakakuta Mwenzao Amefukiwa na Kifusi Kutokana na Bonde Kubwa Alilochimba kwa Shughuli ya Ufyatuaji Tofali.

Katika Hatua Nyingine Mmiliki wa Tofali Hizo Bwana Chesco Mwogofi Mkazi wa Mtaa wa Maheve Amesema Kuwa ni Kweli Kwamba Kijana Huyo ni Mfanyakazi wake Hivyo hadi sasa
Wanaendelea na Jitihada za Kuangalia namna ya Kusafirisha Mwili wa Marehemu baada ya Jeshi la Polisi Kufika na Kuthibitisha Tukio Hilo.

Christopher Mligo ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Maheve Ambaye amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo Ambapo Amesema Kuwa Kama Uongozi wa Serikali umefika Kutoa Taarifa Polisi Ambao Tayari wamefika Katika Eneo Hilo.



 samahani kwa picha hizi za kusikitisha

 Hizi ndizo Tofali zilizokuwa Zikifyatuliwa na Marehemu Pamoja na Vijana Wenzake

 hapa ndipo Mauti Yalipo Mkuta Marehemu Juma Liduke baada ya udongo kumuangukia.
 hawa ndio Vijana waliokuwa wakifanya kazi Pamoja na Marehemu.
 Miongoni mwa Waliokuwa wakifanya Kazi na marehemu Bwana Willy Ndunduru Amesema Marehemu alikuwa Akifanya kazi Karibu na bonde hilo.
 Mmiliki wa Tofali Hizo Ambaye ni Mwajiri wa Vibarua Hao Bwana Chesco Mwogofi Amesema hadi sasa Wanasubiri Kusafirisha Maiti Kwenda Makambako.

 Dokta Omar Kutoka Hospitali ya Mji Njombe Kibena Baada ya Kufika na Maafisa wa Polisi Katika Eneo la Tukio Hilo.

Mwenyekiti wa  Mtaa wa MAHEVE Bwana Christopher Mligo Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles