Freeman Mbowe,Tundu Lisu na Wanasheria Wengine wa CHADEMA KUTUA NJOMBE AGOST 24.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe Akiendeleza Mchakato wa Rasimu ya Katiba.

Tundu Lissu.
Kaimu Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Njombe bwana Alatanga Nyagawa aeleza Ujio wa Viongozi Hao Mjini Njombe Agosti 24 Mwaka Huu.
Agosti 24 Mwaka Huu Viongozi wa CHADEMA Taifa wakiongozwa na Kiongozi wao wa Anga Freeman Mbowe wanatarajia Kutua Mjini Njombe Katika Kuendeleza Mapambano ya Rasimu ya Katiba Mpya.
Kaimu Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Njombe Bwana Alatanga Nyagawa amesema Kuwa Msafara Huo Utatua Mkoani Njombe Ukitokea Mkoani Mbeya Kwa Lengo Kuu la Kuendelea Kukusanya na Kuchambua Rasimu ya Katiba Mpya.
Bwana Alatanga Amesema Kuwa Mkutano Huo Utafanyika Katika Uwanja wa National Housing Mjini Njombe Ukiongozwa na Bwana Mbowe,Tundu Lissu na wanasheria Mbalimbali wa Chadema .