Mpiga Debe asiye na Sare Atakamatwa kwa Uzululaji![]()
Mwenyekiti wa Chama cha Usafirishaji Mkoa wa Njombe Bwana Donatus Mwamanga[DOSMEZA] Aeleza Hali Hilisi ya UsajiriTabia ya Kunyang'anya Mizigo kwa Abiria Imepigwa Marufuku na Hivyo Kuagizwa Kuwa na Sare Kila Kondakta na
Wapiga Madebe.
Katibu wa Kituo cha Mabasi Mjini Njombe Bwana Kelvin Mwarwanda naye Aeleza hatua Hiyo
Na Gabriel Kilamlya Njombe.
Baadhi ya Wamiliki wa Magari Yanayofanya Shughuli za Usafirishaji Abiria Mikoani na Wilayani Katika Kituo Kikuu cha Mabasi Mjini Njombe Wameanza Kutekeleza Agizo la Uongozi wa Kituo Hicho la Kuwasajili Wafanyakazi Wao Ikiwa ni Pamoja na Uvaaji wa Sare na Vitambulisho Hali Ambayo Itasaidia Kupunguza Vitendo Vya Uhalifu Dhidi Abiria na Kuwabaini Watu Wanaojihusisha na Vitendo Hivyo.
Akiongea na Kituo Hiki Mwenyekiti wa Chama cha Usafirishaji Mkoa wa Njombe Donatus Mwamanga Amesema Licha ya Kuanza Kwa Zoezi Hilo Lakini Bado Kuna Changamoto Kadhaa Ikiwemo Baadhi ya Wafanyakazi Kufika Ofisini Kwake Kwa Lengo la Kujisili Bila ya Kuwa na Wajiri Wake Jambo Ambalo ni Kinyume cha Sheria.
Aidha Mwenyekiti Huyo Amewataka Waajiri Kufika Katika Ofisi Yake Akiwa na Wafanyakazi Wake Kwa Ajili ya Kufanya Usajili na Kwamba Kila Gari la Abiria Linatakiwa Kuwa na Wafanyakazi Watatu Tu na Si Vinginevyo.
Kwa Upande wake Katibu wa Kituo Hicho cha Mabasi Kelvin Mwarwanda Amesema Zoezi Hilo Litasaidia Kuwabaini Watu Wanaofika Kituoni Hapo Kwa Lengo la Kufanya Uhalifu na Kuliomba Jeshi la Polosi Kuendelea Kushirikiana na Uongozi wa Kituo Hicho Ili Kukomesha Viendo Vya Uhalifu Dhidi ya Mali za Abiri.
Hivi Karibuni Uongozi wa Kituo Kikuu cha Mabasi Mjini Njombe Kwa Kushirikiana na Jeshi la Polisi Ulitoa Agizo Kwa Wafanyakazi Wote wa Kituo Hicho Kuvaa Sare na Vitambulisho Vinavyoonesha Ofisi Wanazofanyika Kazi Ifikapo Agosti 19 Mwaka Huu na Kwa Yeyote Atakaekaidi Hatua za Kisheria Zitachukuliwa Dhidi Yake