Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 1

$
0
0
BANGI ZAENDELEA KUKAMATWA NJOMBE.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amethibitisha Kutokea kwa Matukio Tofauti Mkoani hapo.


Na Gabriel Kilamlya Njombe

 Licha ya Jitihada Kubwa za Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Kuendelea Kupambana na Watumiaji wa Dawa ya Kulevya Bado Tatizo Hilo Limeonekana Kushika Kasi Mkoani Njombe Siku Hadi Siku.

Siku Chache Zilizopita Jeshi la Polisi Mkoani Hapa Liliripoti  Kuwashikilia Watuhumiwa Mbalimbali Wanaojihusisha na Madawa ya Kulevya Hususani Bangi Pamoja na Kufanikiwa Kuteketeza Kilo 3200 za Bangi Katika Kata ya Matamba Wilayani Makete Huku Matukio Kama Hayo yakiendelea Kujitokeza.

Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe ACP Fulgency Ngonyani Ameeleza Kuwa Jeshi La Polisi Linamshikilia Bahati Moheli Mwenye Umri wa Miaka 25 Ambaye ni Mkazi wa

National Housing Mjini Njombe Kwa Tuhuma za Kukutwa na Bangi Kete Mbili Akiwa na Rafiki yake Chumbani Kwake.

Pamoja na Mtuhumiwa Huyo Kushikiliwa Kwa Kukutwa na Keti za Bangi Agosti 12 Mwaka Huu Majira ya Saa Nane Mchana Lakini Pia Jeshi Hilo Linamtafuta Maulid Ngole Aliyetoroka Mara Baada ya Kukamatwa na Rafiki yake.

Katika Tukio Jingine Mkazi Mmoja wa Kijiji cha Madobe Wilayani Ludewa Thadei Mtitu Mwenye Umri wa Miaka 59 Amekutwa Amefariki Dunia Baada ya Kutumbukia Korongoni.

Kamanda Ngonyani Amesema Kuwa Tukio Hilo Limetokea Agosti 12 Mwaka Huu Majira ya Saa Nne Asubuhi Baada ya Mkazi Huyo Kuteleza na Kutumbukia Kwenye Korongo Hilo Wakati Akichunga Mifugo yake.

Pamoja na Matukio Hayo Lakini Pia Kamanda Ngonyani Amewataja Majeruhi Wanne wa Ajali  ya Gari Iliyoacha Njia na Kupinduka Katika Kijiji cha Lusisi Wilayani Wanging'ombe.

Amesema Kuwa Tukio Hilo limetokea Agosti 12 Mwaka Huu Majira ya Saa 8:25 Mchana Katika Kijiji Hicho Baada ya Gari Lenye Namba za Usajili T 270 BPG Aina ya ROSA Mali ya Andrew Mbilinyi Mkazi wa Makambako Iliyokuwa Ikiendeshwa na Henry Nyekelele Mwenye Umri wa Miaka 42 Ambaye naye ni Mkazi wa Makambako Kuacha Njia na Kupinduka na Kusababisha Majeruhi Wanne Ambao Wanaendelea na Matibabu Katika Hospitali ya Kibena Mjini Njombe.

Aidha Amewataja Majeruhi Hao Kuwa Ni Ziada Kawogo Mwenye Umri wa Miaka 25 Mkazi wa Makambako,Paul Mshedu (70)  Mkazi wa Mahaji,Beltha Nyamle(42) Mkazi wa Mlowa Iringa na Felista Msigwa Mwenye Umri wa Miaka 35 Ambaye ni Mkazi wa Mlevela.

Hata Hivyo Kamanda Ngonyani Amesema Kuwa Jeshi la Polisi Linamshikilia Dereva Huyo na Kwamba Chanzo cha Ajali Hiyo ni Kuchoma kwa Mkono wa Usukani.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles