WANAFUNZI WA SEKONDARI YA JOSEPH MBEYELA HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MLIPUKO KWA UPUNGUFU WA VYOO MJINI NJOMBE.![]()
![]()
Na Gabriel Kilamlya
Kwasasa Shule Hiyo Ina Wanafunzi Mia Sita wa Kidato Cha Kwanza Hadi Cha Nne Huku Ikiwa na Matundu Nane ya Vyoo Yakiwemo Manne Kwaajili ya Wasichana na Manne Kwaajili ya Wavulana.
Makamu Mkuu wa Shule Hiyo Bw Rashidi Kinyaga Anakiri Kuwepo Kwa Tatizo Hilo na Kusema Kuwa Ili Kuhakikisha Wanamaliza Tatizo Hilo,Uongozi wa Shule Umewataka Wazazi Kuchangia Shillingi Elfu Kumi Kila
Mmoja Kwaajili ya Ujenzi wa Vyoo Hivyo.
Amesema Kwa Kutambua Hatari Inayowakabili Wanafunzi Hao Uongozi wa Shule Umekuwa Ukisisitiza Umuhimu wa Wazazi Hao Kuchangia Fedha Hizo Ambazo Zitasaidia Kuongeza Idadi ya Matundu Hayo na Kuboresha Huduma ya Choo Shuleni Hapo.
Venance Msungu ni Afisa Elimu Secondary Halmashauri ya Mji wa Njombe Anakiri Kuwepo Kwa Tatizo Hilo na Kusema Serikali Imeanza Kuchukua Hatua Kadhaa Ili Kukabiliana na Tatizo Hilo.
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Hali ya Elimu,Mkoa wa Njombe Una Mahitaji ya Matundu Zaidi ya Elfu Moja Kwaajili ya Wavulana na Zaidi ya Elfu Moja Kwaajili ya Wasichana Wakati Halmashauri ya Mji Njombe Ikiwa na Mahitaji ya Zaidi ya Matundu Mia Moja Kwaajili ya Wasichana na Zaidi ya Mia Mbili Kwaajili ya Wavulana.