Hili ni Jengo la Zahanati ya Mtaa wa SIDO Ambalo limesimama baada ya Kukosa Bati takribani 50 Kutokana na Kufika CHACHE Toka kwenye Mfuko wa Jimbo.
Hili ni eneo la Jengo la Zahanati lililokosa Bati za Kukamilisha Baada ya Kufika 150 Kati ya 200 Wanazodai waliahidiwa na Mbunge wao.
Hivi Ndivyo Ilivyo katika Zahanati Hiyo Mjini Njombe na Hapo ni sehemu ya Katikati iliyosalia Kukamilika mara baada ya Kufeli kwa Bati.
Na Gabriel Kilamlya Njombe.
Serikali Mjini Njombe Imetoa Ufafanuzi Kuhusu Ujenzi wa Zahanati ya Mtaa wa SIDO Ambayo Ujenzi Wake Umesimama Kwasasa Kutokana na Kukosekana Kwa Bati Kwaajili ya Upauaji.
Aidha Pamoja na Ufafanuzi Huo Pia Serikali Imewataka Wananchi Kuendelea Kuchangia Ujenzi wa Zahanati Hiyo Badala ya Kuendelea Kusubiri Ahadi za Wanasiasa Ambazo Zimekuwa Hazitekelezwi Kwa Wakati.
Afisa Mipango Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Sadolt Kaijage Amesema Ahadi ya Kuchangia Bati Kwaajili ya Ujenzi wa Zahanati Hiyo Ulikuwa ni
Uamuzi wa Kamati ya Jimbo la Njombe Kusini na Kusema Kuwa Haikuwa Ahadi ya Mbunge Hivyo Wananchi Wanapaswa Kushirikiana na Serikali Katika Kuchangia Ujenzi Huo.
Wakizungumza na Uplands Fm Baadhi ya wananchi wa Mtaa Huo walidai Kuwa Licha ya Kuomba Bati Mia Mbili lakini wamepata Bati 150 ambazo zimeshindwa Kukamilisha Zoezi la Upauaji wa Zahanati Hiyo.