Watu 9 familia mbili tofauti wamenusurika kifo kufuatia ajali ya moto uliotokea na kuunguza nyumba wanayo ishi katika mtaa wa Makongoro manispaa ya Morogoro huku samani za ndani zikiteketea kabisa licha ya jeshi la zimamoto na uokoaji kufika katika eneo la tukio kwa wakati na kufanikiwa kuuzima moto huo.
Ramadhani Pilipili ni kamishina msaidizi kamanda wa zimamoto na uokoaji mkoa wa morogoro ambaye ameelezea hali ya moto huo huku akiendelea kuwashauri wananchi kuwasiliana na jeshi hilo mapema yanapo tokea majanga ya moto.