Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Karatasi za kupigia kura Kenya zimefutwa

$
0
0

Mahakama kuu nchini Kenya imefuta karatasi za kupigia kura na kuamrisha mchakato wa uchapishaji wa karatasi hizo kurudiwa upya.
 
Na Gabriel Kilamlya NAIROBI

Mahakama kuu nchini Kenya imefutilia mbali zabuni ya jumla ya Uro Milioni 24   ya uchapishaji wa karatasi za kura ya urais nchini humo.

Mahakama imechukua hatua hiyo ikitoa uamuzi kuhusu kesi iliyowasilishwa na upinzani kupinga utoaji wa zabuni hiyo.

Upinzani ulikuwa umesema kampuni iliyopewa kandarasi hiyo ina uhusiano na Rais Uhuru Kenyatta amabye pia anawania katika uchaguzi huo utakaofanyika tarehe 8 Agosti.

Jopo la majaji watatu limesema Tume Huru ya Uchaguzi  ilikosa kushauriana na wagombea wote wa uchaguzi huo kabla ya kukabidhi zabuni hiyo kwa Al Ghurair ya Dubai.

Mahakama imeamua kuwa zabuni hiyo itangazwe upya.

Muungano mkuu wa upinzani National Super Alliance (Nasa), ulikuwa umewasilisha kesi kortini ukisema kampuni hiyo ilipewa zabuni hiyo bila utaratibu unaofaa kufuatwa.

Kampuni ya Al Ghurair na Bwana Kenyatta wote wamekana kuwa na uhusiano wowote.

Mahakama iliamua kwamba kampuni hiyo inaweza kuchapisha karatasi za uchaguzi wa wabunge na maseneta, madiwani na magavana, ambao pia utafanyika tarehe 8 Agosti.

Mgombea urais wa Nasa Raila Odinga anashindana vikali na Rais Kenyatta, katika kinyang'anyiro ambacho ni kama marudio ya uchaguzi wa mwaka 2013.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles