Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

WAKAZI WA KIJIJI CHA INYAMALO NJOMBE WAOKOA ZAIDI YA TSH.45 MILIONI UJENZI WA NYUMBA YA MWALIMU

$
0
0
 Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka Akikagua Ujenzi wa Nyumba ya Pili ya Walimu Katika Shule ya Msingi Inyamalo
 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Chidtopher Ole Sendeka Akiweka Jiwe la Msingi Katika Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu Katika Shule ya Msingi  Inyamalo .
 Wananchi wa Inyamalo Wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Njombe.


 Wakazi wa kijiji cha Inyamalo wakimsikiliza mkuu wa Mkoa wa Njombe Alipofika Kwa Ziara ya Kikazi Kijijini Hapo.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akizungumza na wakazi wa kijiji cha Inyamalo Wilayani Njombe

Na Gabriel  Kilamlya NJOMBE

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka Amewataka Wananchi wa Vijiji Mbalimbali Wanaoendelea Kujenga Miradi Mbalimbali ya Maendeleo Kuiga Mfano wa Wakazi wa Kijiji Cha Inyamalo Wilayani Njombe  Ambao Wamejenga Za walimu na Kuokoa Fedha Nyingi Kwa Kujenga Nyumba Nzuri ya Mwalimu Kwa Gharama Ndogo.

Kauli Hiyo Ameitoa Wakati Akiweka Jiwe la katika Nyumba ya Mwalimu Katika Shule ya Msingi Inyamalo Inayojengwa Kwa

Nguvu za Wananchi Pamoja na Serikali Inayotarajia Kutumia Takribani Shilingi Milioni 25 Hadi Kukamilika Kwake.

Taarifa ya Ujenzi wa Nyumba Hiyo Iliyosomwa na Mwalimu Mkuu wa Shule Hiyo Bwana Florence Nzalalila Imeeleza Kuwa Licha ya Ujenzi Huo Kufikia Hatua ya Upauaji Lakini Ilipaswa Kuwa Imekamilika.

Walimu wa Shule ya Msingi Inyamalo Wamesema Kujengwa Kwa Nyumba Hizo Kutawasaidia Kuishi Jirani na Shule Ikiwa ni Pamoja na Kuokoa Gharama za Kulipia Kodi ya Pango Ambazo Wamekuwa Wakilipa Hadi Sasa.

Tatizo la Uhaba wa Nyumba za Walimu Limeonekana Kuwa Kubwa Zaidi Kutokana na Baadhi ya Shule Kukosa Nyumba za Walimu Hapa Nchini Kwa Muda Mrefu .

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles