KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI CHAPEWA MAELEZO TOFAUTI JUU YA MWANAFUNZI KUZAMA KWENYE BWAWA MATEMBWE NJOMBE.
Picha toka Maktaba yetu ya Msanii wa Kibena aliyezama kwenye Maji katika Bwawa la TANWATT Kibena Njombe wakati akitolewa kwenye maji tukio linalofanana na Hilo.
Na Gabriel Kilamlya.
Kikosi cha Zima moto na Uokoaji Mkoa wa Njombe Kimeshindwa Kumuokoa Mwanafunzi wa darasa la saba mwenye umri wa miaka 13 katika shule ya msingi Matembwe Filbert Luwanja Ambaye anadaiwa kuzama Kwenye Maji ndani ya Bwawa tangu Jana.
Kushindwa Kwa Kikosi Hicho kwa Siku ya Leo Licha ya Kufika Katika Eneo la Tukio Kumetokana na Kupokea Taarifa tofauti ambapo Kama zima Moto na Uokoaji Walijulishwa Kuwa Mtoto Huyo alizama Kwenye Kisima wakati ni Bwawa na Hivyo walipofika wakawa na Vifaa vya Kuokoa kwenye Kisima kwa Lengo la Kutaka Kukausha Maji na Ndoano tu.
Akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Mwenyekiti wa Kitongoji cha Itundu bwana Katika Kijiji cha Matembwe Bwana Justin Mfugale amesema kuwa taarifa za kuzama kwa mtoto huyo tayari zimefikishwa katika kituo cha polisi Lupembe na
kwamba jitihada mbalimbali zinaendelea za kumtafuta mtoto huyo.
Aidha Amesema Kuwa Mara Baada ya Kufika Kwa Askari Hao watatu na Gari Hilo wakashindwa Kufanya chochote zaidi ya Kupima Kina cha Maji Katika Bwawa Hilo lililopo Katika Kijiji cha Matembwe na Kuondoka.
Daniel Nyarusi ni Mwenyekiti wa kijiji cha Matembwe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mpaka sasa wataalamu mbalimbali wa kuogelea wanaendelea kumtafuta mtoto huyo kwenye bwawa la maji hilo.
Aidha bwana Nyarusi amesema kutokana na jitihada za kuogelea kutozaa matunda tangu jana walipoanza kuogelea kutafuta mtoto huyo aliyezama kwenye maji hayo ameiomba halmashauri ya wilaya ya Njombe kuwasaidia wataalamu ambao wanauwezo wa kuzama ndani ya maji ili kumtafuta mtoto huyo anadaiwa kuzama ndani ya maji hayo.