Balozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia anakabiliwa na notisi ya kuondoka nchini humo kufuatia mgogoro kuhusiana na uchunguzi wa kifo cha Kim Jong nam nduguye wa kambo rais wa Korea kaskazini.
Mamlaka ya Malaysia imeishtumu Pyongyang kwa kujaribu kuingilia uchunguzi huo.
Korea Kaskazini nayo imekataa ripoti ya upasuaji ambayo inaonyesha kuwa King Jong nam alifariki baada ya wanawake wawili kumpaka sumu aina ya VX aktika uso wake.