Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

WATATU WAFA KWA AJALI NJOMBE

$
0
0

Dennis Mwalongo


Watu watatu wamefariki na 34 wamejeruhiwa akiwemo mwananke mmoja mjazito katika ajali ya basi la kampuni ya ILYANA yenye namba za usajili T 202 DGK inayofanya safari zake kutoka jijini Dar es salaam mpaka mjini songea mkoani Ruvuma. Ajali hiyo imetokea majira ya saa tatu usiku wa kuamkia machi tatu katika kjiji cha Igominyi halmashauri ya mji wa Njombe na kugharimu maisha ya watu watatu papo hapo huku chanzo chake kikielezwa kuwa ni mwendo kasi.

 Mwenyekiti kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka amesema kuwa Dereva aliyesababisha ajali na kukimbia anatufutwa ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria. Kaimu mganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Njombe Kibena Isaya Mvinge amesema kuwa utambuzi wa miili ya waliofariki umefanyika ambapo watu wawili wametambuliwa akiwemo mfanyakazi wa Wakala wa kununua nafaka NFRA Pindaheri Jacobu Singa Ruvuma huku akibainisha kuwa mwananmke alipata ajali akiwa mjazito amefanyiwa oparesheni na mtoto anaendelea vizuri. 

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI.....................

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles