Na Gabriel Kilamlya
Wakati Maonyesho ya Siku ya Wakulima Maarufu Kama Nanenane Yakitarajiwa Kuanza Kote Nchini Agosti Mosi Mwaka Huu Baadhi ya Halmashauri za Mkoa wa Njombe Zimeelezea Changamoto Kadhaa Zinazozikabili Halmashauri Hizo Ikiwemo Uhaba wa Vyombo Vya Usafiri.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Sengayavene Mkalimoto Amesema Licha ya Maandalizi Kwa Ajili ya Maonesho Hayo yakiendelea Lakini Bado Suala la Usafiri Limeonekana Kuwa Tatizo Hasa Katika Kuwasafirisha Washiriki wa Maonesho Hayo Kutoka Wilayani Njombe Kuelekea Mkoani Mbeya.
Amesema Kutokana na Tatizo Hilo Tayari Halmashauri Hiyo Imetoa Wito Kwa Washiriki Ambao Wanauwezo wa Kujigharamia Wenyewe Ili Kuweza Kushiriki Maonyesho Hayo Kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Yatakayofanyikia Mkoani Mbeya.
Kwa Upande Wake Mratibu wa Maonyesho ya Nanenane Kwa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Victor Luvinga Amesema Maandalizi Katika
Halmashauri Hiyo Yanaendelea Vizuri na Tayari Wamewaalika Wadau Mbalimbali Kushirika Maonyesho Hayo
Maonyesho ya Nanenane Kitaifa Yatafanyikia Mkoani Dodoma Viwanja Vya Nzunguni Yakiwa na Kauli Mbiu Isemayo Zalisha Mazao ya Kilimo na Mifugo Kwa Kulenga Mahitaji ya Soko, Ambapo Kwa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini Yatafanyikia Mkoani Mbeya Kwenye Viwanja Vya John Mwakangale.
.............................................................................................................