Na Mboza Lwandiko
Lipa Kodi ya Ardhi kwa wakati, uepuke kutozwa Tozo, Kutangazwa kwenye Vyombo vya Habari, Kupelekwa Mahakamani na Kufutiwa umiliki wa ardhi yako, kwani Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 inaainisha gharama hizo kwa wasiozingatia ulipaji Kodi.
kutozingatia kulipa Kodi ya pango la Ardhi kwa wakati, ambapo mmiliki asiyezingatia hilo kwanza; atatozwa Tozo na baadae Kupelekewa hati ya madai na kufikishwa Mahakamani kulingana na kifungu Na. 50 na hatimaye kufutiwa umiliki wa ardhi kulingana na Sheria hiyo hiyo katika kifungu Na. 49-51.
Akizungumza na Waandishi wa habari hivi karibuni wakati wa zoezi la kutoa notisi ya siku 14 kwa wadaiwa sugu wa Kodi ya Pango la Ardhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila amesisitiza kwa umma kuwa wadaiwa wote wa Pango la Ardhi wamekumbushwa na Serikali kwa muda mrefu, na hivyo ni wakati wao kuhakikisha wanalipa madeni yao yote ipaswavyo.
Aliendelea kusema kuwa; kwa Mwaka wa fedha 2016/17 Wizara imepanga kukusanya Sh. bilioni 111.77 kutokana na Kodi ya Pango la Ardhi.
Dkt. Kayandabila alisema kwakuwa Kodi ya Ardhi inatambulika bayana chini ya Sheria, kila mmiliki wa Ardhi hana budi kuzingatia hilo. Malipo ya pango la ardhi yanatozwa kwa wamiliki wa viwanja na mashamba yaliyopimwa na kumilikishwa kisheria.
Pia mtu yeyote anayemiliki ardhi iliyopimwa kisheria iwe imeendelezwa au haijaendelezwa bado anapaswa kulipa kodi ya pango. Kila mmiliki anaongozwa na mkataba wa kulipia kodi ya pango la ardhi kila mwaka tarehe 1 (Mosi) Julai, Sheria ya Ardhi Na.4 ya mwaka 1999 kifungu cha 33 na kifungu kidogo cha 11 imetoa mwanya kwa walipa kodi kuendelea kulipa bila adhabu hadi tarehe 31 Desemba ya mwaka unaohusika. Baada ya hapo adhabu inatozwa. Mteja anapaswa kufanya malipo ya Kodi ya pango la Ardhi kwa kuwa ananufaika na matumizi ya ardhi hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akiongea na waandishi wa habari kwamba Serikali kupitia Wizara yake haitamuacha mtu au kampuni yoyote inayodaiwa kodi ya Ardhi hata kama ni Taasisi ya Serikali.
Watumishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment wakiwa nje ya ofisi Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) ili kuwasilisha notisi ya madai ya kodi ya ardhi.
Wafanyakazi wa Lamada Hotel (kushoto) wakiangalia kwa makini Notisi ya madai ya kodi ya Ardhi wakati ikiwasilishwa na watumishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment.