Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 0

$
0
0

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu Ofisini Kwake Juu ya Watuhumiwa hao Leo.

Na Michael Luoga.

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linawashikilia Watu Watatu  Samweli Mkongwa , Siri Mtema na Stewart Kiwiki Wakazi wa Wilaya ya Njombe Kwa Tuhuma za Mauwaji ya Stephano Mtela Mwenye Umri wa Miaka 65 Mkazi wa Kijiji cha  MtulingalaKamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amesema

Tukio Hilo LImetokea Julai 22 Mwaka Huu Majira ya Saa Moja na Dakika 30 Asubuhi  na Kwamba Marehemu Alikutwa Ameuwawa Kwa Kukatwakatwa na Kitu Chenye Ncha Kali Sehemu za Kichwani  na Mgongoni .Kamanda Ngonyani Amesema Chanzo cha Mauaji Hayo ni Imani za Kishirikina

Aidha Jeshi Hilo Limethibitisha Kutokea Kwa Kifo cha Mtoto Aziza Malekela Mwenye Umri wa

Mwaka Moja Mkazi wa  Lujewa Mkoani Mbeya Baada ya Kugongwa na Gari Aina ya Landlover Lenye Namba za Usajili  T 627 AMD Linalomilikiwa na Kuendeshwa na Joel Chungwa Mkazi wa Ninga.

ACP Ngonyani Amesema Tukio Hilo Limetokea Julai 22 Mwaka Huu  Majira ya Saa Mbili  Asubuhi  Katika Kijiji cha Ilengititu Halmashauri ya Mji wa Makambako .

Amesema Chanzo cha Ajali Hiyo ni Ubovu wa Barabara Hali Iliyopelekea Gari Hilo Kushindwa Kupanda Mlima na Kuanza Kurudi Nyuma na Kugonga Ukingo wa Barabara na Kisha Kusababisha Ajali Hiyo, na Kwamba Dereva wa Gari Hilo Amekimbia Mara Baada ya Kutokea Kwa Ajali Hiyo.

Katika Tukio Jingine Kamanda Ngonyani Amesema Watu Wanne Wanaodhaniwa Majambazi Walivamia Nyumba ya Lwidiko Myale  Mkazi wa Ngamanga  na Kumjeruhi Kwa Kumkata Kwa panga Sehemu za Kichwani na Kisha Kuiba Fedha Zilizokuwa Ndani  ya Jaketi Ambazo Thamani Yake Hazikufahamika Mara Moja.

Kamanda Huyo wa Polisi Amesema Tukio Hilo Limetokea Jana Majira ya Saa Sita Usiku , na Kuongeza Kuwa Majeruhi Amelazwa Katika Kituo cha Afya Makambako Akipatiwa Matibabu na Hali Yake Inaendelea Vizuri.

Jeshi  la Polisi Mkoani Njombe Linaendelea na Upelelezi Ili Kuwabaini Wahusika wa Matukio Hayo Huku Likiwaomba Wananchi Kutoa Ushirikiano Kwa Jeshi Hilo Kwa Lengo la Kukomesha Vitendo Vya Uhalifu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles