WAZIRI WA MAMBO YA KATIBA NA SHERIA HARISON MWAKYEMBE BAADA YA KUWASILI MKOA WA NJOMBE KATIKA ENEO LA UKUMBI WA CHUO CHA MAENDELEO NJOMBE MJINI AKISALIMIANA NA WAKUU WA WILAYA ,WAKURUGENZI NA WATALAAMU MBALIMBALI WA MIKOA YA NJOMBE NA IRINGA
Na Michael Ngilangwa NJOMBE
Waziri wa Katiba na Sheria Dokta Harison Mwakyembe leo amekabidhi Tuzo Katika Halmashauri na mikoa ya Njombe na Iringa ambayo imepata asilimia 98 Kwa kuongoza katika zoezi la usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ulioendeshwa chini ya Wakala wa Usajiri, Ufilisi na Udhamini RITA.
Waziri Mwakyembe Amekabidhi Tuzo Hizo kwa Halmashauri za Mkoa wa Njombe Na Iringa baada ya kuongoza katika zoezi hilo la usajili wa vyeti vya kuzaliwa na kupongeza kwa hamasa iliyofanyika kwa mikoa hiyo ambayo miaka michache iliyopita maendeleo ya Usajili yalikuwa Duni ambapo Njombe ilikuwa asilimia nane na sasa imefikia asilimia 98.
Waziri Mwakyembe Amesema Mikoa ya Njombe Na Iringa Imechangia kuijengea misingi imara ya maendeleo ya Nchi na kusema kuwa nchi yoyote ili ifanikiwe lazima iwe na takwimu sahahi za wakazi wake na kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo ya kuanzisha Viwanda katika kuelekea Uchumi wa Kati wa Nchi ya Tanzania.
Amesema Mikoa Mingine ya Tanzania Inapaswa Kutembelea Mikoa ya Njombe na Iringa Ili Kujifunza namna ilivyofanikiwa katika kutekeleza zoezi la kuhamasisha wananchi kupeleka watoto wao kuwasajili na kusema jitihada hizo Zinatakiwa Kuendelee kufanyika hata kwa mikoa mingine kufikia asilimia walizopata mikoa ya Njombe na Iringa.
Akisoma Taarifa Fupi Mbele ya Mgeni Rasmi Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Harison Mwakyembe ,Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa usajiri,Ufilisi na Udhamini RITA Bi. Emmy Hudson amesema Mkoa wa Njombe Na Iringa imeweza kuvuka malengo ya kusajili na kuwapa vyeti vya kuzaliwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano Ambapo RITA Imeamua kupongeza mikoa iliyofanya vizuri Ili kuwa mfano kwa Mikoa mingine.
Kwa Upande Wao Wakuu wa Mikoa ya Njombe Na Iringa Christopha Ole Sendeka na Amina Masenza Wameshukuru kwa kupewa zawadi hizo na kusema mpango wa kusajili watoto ulianza mwezi Decemba 22 ,2016 zikitolewa kwenye ofisi za watendaji wa kata na vituo vya tiba za mama na mtoto nakwamba usajili huo sasa utakuwa ni agenda ya kudumu Na kulishukuru shirika la Unisef kwa kuwa mdau katika zoezi hilo.
WAZIRI WA MAMBO YA KATIBA NA SHERIA HARISON MWAKYEMBE AKIWA UKUMBINI
MKUU WA MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA OLE SENDEKA