Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 0

$
0
0
 WAFANYABIASHARA NJOMBE WAHAKIKISHIWA ULINZI NA USALAMA KTK BIASHARA ZAO.
 Meneja Uhusiano Mikopo NMB Makao Makuu Bwana Dickson Pangamawe akiwasilisha Mada Kwa wanachama wa NMB BUSINESS CLUB Njombe leo wakati wa mkutano wa Pili wa Club Hiyo.
 Kamanda Ngonyani Akiwahakikishia Ulinzi na Usalama wafanyabiashara Mkoani Njombe Leo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bi.Dolkas Mkelo akiwasilisha Mada Juu ya Mazingira ya
Kibiashara kwa Wafanyabiashara Mjini Njombe.



 Viongozi wa NMB BUSINESS CLUB Mkoa wa Njombe Wakiwa Kwenye Picha ya Pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani Baada ya Kuwasilisha Mada ya Ulinzi na Usalama kwa Wafanyabiashara Mkoani Hapa leo.


 Wanachama wa NMB BUSINESS CLUB Mkoa wa Njombe wakiwa Kwenye Picha ya Pamoja Mara baada ya Kumalizika kwa Mkutano wa Pili wa Club Hiyo.

Gabriel Kilamlya Na Prosper Mfugale.

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limewahakikishia Wafanyabiashara Kuwa Litaendelea Kuimarisha Hali ya Ulinzi na Usalama na Kupambana na Matukio ya Uhalifu Yanayoweza Kuhatarisha Ustawi wa Biashara Mkoani Njombe.

Miongoni Mwa Hatua Zilizochukuliwa na Jeshi Hilo Katika Kuimarisha Ulinzi ni Pamoja na Kuweka Askari Katika Kata na Tarafa Zote Mkoani Hapa.

Akizungumza Wakati wa Semina ya Wanachama wa NMB Club Mjini Njombe Jana,Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe Fulgency Ngonyani Amesema Pamoja na Mambo Mengine,Jeshi Hilo Pia Kwa sasa Limeanza Kutoa Huduma ya Kusindikiza Fedha Benki Kwa Gharama ndogo Hali Ambayo Inawahakikishia Wafanyabiashara Usalama wa Fedha Zao

Dickson Pangamawe ni Afisa Uhusiano wa Mikopo NMB Makao Makuu Anasema Bado Kumekuwa na Changamoto ya Wateja Kushindwa Kurejesha Mikopo Kwa Wakati na Kushindwa Kutumia Mikopo Hiyo Kwa Malengo Yaliokusudiwa.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa NMB CLUB Mkoa wa Njombe Bwana Vikael Sanga amesema kuwa Kuanzishwa kwa Club hiyo Kumekuwa na Mafanikio Kadhaa Miongoni Mwa Wanachama ikiwemo Kufanyiwa Kazi Kwa Baadhi ya Kero za Wateja.

Hemed Risasi ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Njombe ambaye amesema Kutokana na Usumbufu unaojitokeza Mara kwa mara kwa wateja hususani katika Huduma ya ATM Benki hiyo imeendelea Kuboresha Huduma zake kwa Njia ya Huduma mbalimbali za Simu kama kutoa au Kuweka fedha kwenye akaunti kwa njia ya M Pesa,Tigo Pesa pamoja na Air tel money .

Ameongeza kuwa katika adha hiyo wameanzisha Huduma ya JISEVIE Kwa kutumia Mitandao ya simu.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles