Mahakama ya wilaya ya njombe imeendelea kusikiliza kesi ya ku-uwa bila kukusidia, inayomkabili Hilolusi Mwapinga mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa Lusitu mkoani Njombe.
Akisoma Hati ya mashitaka Mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo John Kapokolo, mwendesha mashtaka Selapiani Matiku ameiambia mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Mnamo March 7 mwaka 2o11 katika kijiji cha Lusitu mkoani Njombe.
Imedaiwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alifanya Unyama Huo, mnamo tarehe 7 march mwaka juzi majira ya saa nane mchana, katika kijiji cha Lusitu mkoani njombe, Ambapo alimpiga kwa kitu kizito Castory Muhinga mkazi wa
kijiji cha Lusitu na kumsababishia kifo Papo Hapo.
Matiku Ameongeza Kuwa, mshitakiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani hapo mnamo terehe 10 mwezi wa 3 mwaka 2011, na baada ya kusomewa shitaka linolo mkabili alikil i kutenda kosa hilo mbele ya mahakama.
Kwa Mujibu wa Mwendesha Mashtaka wa Upelelezi wa Kesi Hiyo, Tayari Umekwishakamilika, na Jumla ya Mashahidi 13 Wanatarajiwa Kutoa Ushahidi Wakati Kesi Hiyo Itakapoanza Kusikilizwa Katika Mahakama Kuu.
Wakati Huo Huo, Mkazi wa Mtaa wa Kawawa Mjini Makambako Rehema Nyagawa, Jana Amefikishwa Katika Mahakama ya Wilaya ya Njombe na Kusomewa Shitaka la Kujipatia Fedha Kiasi cha Shilingi Milioni 10 Kwa Njia ya Udanganyifu, Kutoka Kwa Bi. Salome Kyusa.
Akisoma Hati ya Mashtaka Mbele ya Hakimu wa Mahakama Hiyo John Kapokolo, Mwendesha Mashtaka Serapian Matiku Ameiambia Mahakama Kuwa, Mshtakiwa Alitenda Kosa Hilo Mnamo Julai Kumi Mwaka Huu Akiwa Katika Mji Mdogo wa Makambako.
Hata Hivyo Hakimu John Kapokolo ameahirisha kesi hiyo hadi Agost 19 mwaka huu, Ambapo mshtakiwa Ametakiwa kufika mahakamani Hapo na mashahidi wa Tuhuma Hiyo.
..........................................................................................................................