Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

RC MASENZA AKWEPA ADHABU YA RAIS DR MAGUFULI ,ATEKELEZA AGIZO LA MADAWATI

$
0
0


Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa  Amina Masenza  akitazama  madawati  yaliyokamilika kulia ni  afisa  habari wa Manispaa ya  Iringa  Sima Bingileki

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza  kulia  akimkabidhi  madawati 100  mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Bw. Ahmed  Sawa   leo baada ya  mkoa kukamilisha utekelezaji wa agizo la Rais kuhusu madawati 
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya  wilaya ya  Kilolo kulia  akipokea madawati  kutoka kwa  mkuu wa mkoa wa Iringa
Mwakilishi  wa mkurugenzi wa Halmashauri ya  Wilaya ya  Iringa Bi  Hawa akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Masenza mara  baada ya  kukabidhiwa madawati


Na MatukiodaimaBlog

SERIKALI    ya    mkoa wa  Iringa  imetekeleza  agizo la  Rais  Dr  John Magufuli  kwa kukabidhi  jumla ya madawati 21,304 kwa   shule  za  msingi  na   sekondari katika Halmashauri  zote  tano  za  mkoa   huo .

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Bi  Amina  Masenza  akikabidhi  mgao wa  madawati hayo kwa  wakurugenzi wa Halmashauri   hizo leo  zoezi  lililofanyika kwenye  karakana na  chuo  cha  ufundi  stadi  VETA , alisema  kuwa  utekelezaji  wa  agizo  hilo  umefanikiwa  kutokana na  mwitikio mzuri  wa  wananchi  wa  mkoa  huo  na  wadau mbali  mbali wa  maendeleo  ambao  kwa  umoja  wao wamesaidia zoezi hilo  kukamilika .


Alisema  kuwa Rais Dr  Magufuli  alitoa  agizo kwa  wakuu  wote wa  mikoa  nchini kuhakikisha  wanafunzi wote wanakaa katika madawati  ifikapo leo  Juni 30  mwaka  huu na  kuwa  kutokana na agizo hilo alilazimika  kuwashirikisha   wakuu  wake  wa  wilaya  na  wadau mbali  mbali  wakiwemo  wananchi  mmoja  mmoja na  kila  mmoja kwa  uwezo  wake  aliweza  kuchangia madawati hadi  kufanikisha  zoezi hilo.


Mkuu  huyo  alisema kwa Halmashauri za  mkoa wa  Iringa zimetengeneza madawati  kupitia  bajeti  zake  na  wadau  waliopo kwenye  Halmashauri   husika  na  kuwa  hadi sasa  mkoa   umetekeleza  kutengeneza madawati hayo 21,304 wakati  madawati 3665  huku   madawati  8,163 kwa  ajili ya  shule za msingi  wakati  madawati  1,264  ya  shule za  sekondari  yanaendelea  kutengenezwa  katika karakana  mbali mbali   na  fedha  kwa  ajili ya matengenezo hayo  tayari  zimelipwa .

Hivyo  alisema  madawati  yanayoendelea kutengenezwa  yanatarajiwa   kukamilika July 15 mwaka  huu kwani  yamechelewa  kukamilika  kutokana  na  wakandarasi wanaotumika  kutengeneza  madawati  hayo  kuwa na kazi  nyingi .



Bi Masenza  alisema  kuwa  ofisi  yake  kwa  kushirikiana na  wadau  mbali mbali imeweza kutengeneza  madawati 700 kwa  lengo la  kuunga mkono  jitihada za  Halmashauri za kumaliza tatizo  la  madawati mapema ,ambayo yamegawiwa  katika Halmashauri tano za  mkoa wa  Iringa ambazo ni Iringa Manispaa madawati 200, Mji Mafinga  madawati 100 ,Halmashauri ya Iringa madawati 100 ,halmashaur i ya  Mufindi madawati 100 na  Kilolo madawati 100

Wakati  madawati  308 yanaendelea   kutengenezwa  katika karakana ya  VETA  pindi yatakapokamilika  yatafikisha idadi ya madawati 1,008  jumla ya  fedha  ambazo zimetumika  kutengeneza  madawati  hayo 1,008 ni milioni 50,400,000 na  baada ya madawati  yote  kukamilika   kutengenezwa mkoa  wa Iringa hautakuwa na  upungufu wa madawati  kwa  wanafunzi  zaidi ya  kuwa na ziada ya madawati .


Mkoa  wa  Iringa  una jumla ya   shule  za msingi 478 na  shule za  sekondari 107zinazomilikiwa na  serikali  na  mkoa  huo  ulikuwa na  upungufu wa madawati 29,347  ikiwa ni madawati 26,046 ya  shule  za Msingi na madawati  3301 kwa  shule za  sekondari.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles