Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

DC WANGING'OMBE ATOA SIKU 7 KWA WAKUU WA SHULE KUHAKIKISHA WATOTO WANARIPOTI SHULENI

$
0
0

 Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Dokta Asumpta Mshama wa pili kulia akizungumza kwenye kikao cha Wakuu wa shule za sekondari



Baadhi ya Wakuu wa Shule za Sekondari na Wenyeviti wa Bodi Wakiwa na Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Dokta Asumpta Mshama

Na Gabriel  Kilamlya Wanging'ombe

Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Dokta Asumpta Mshama  Amesema Yuko Tayari Kupelekwa Mahakamani na Tume ya Maadili ya Walimu TSD Wilaya Hiyo Kwa Kuagizwa Kusimamishwa Kazi Mwalimu wa Shule ya Sekondari Ilembula Ambaye Anatuhumiwa Kujihusisha Kimapenzi na Mwanafunzi na Kumsababishia Kufeli Mtihani.

Dokta Mshama Ametoa Kauli Hiyo Jana Wakati Akizungumza na Wenyeviti wa Bodi za Shule za Sekondari na Wakuu wa Shule Zote za Wilaya Hiyo Katika Kujadili Tathimini ya Hali ya Elimu Katika Wilaya Hiyo.

Amesema Baadhi ya Walimu Wamekuwa Wakifanya Mapenzi na Wanafunzi na Hatimaye Wanashindwa Kuwajibishwa Kutokana na Mzunguko Mrefu Kupitia TSD Ambao Wanashindwa Kufuatilia Kwa Wakati Matatizo Hayo Kwa Kukosa Fedha.

Aidha Amesema Hayuko Tayari Kuona Mwalimu Huyo Anaendelea Kufundisha Katika Shule za Wilaya Hiyo Kabla Kesi Yake Haijaisha Hadi Pale TSD Itakapopata Fedha za

Kuwalipa Posho Wajumbe Watakaokwenda Kufuatilia Suala Hilo.

AKitolea Ufafanuzi Suala Hilo Kaimu Katibu wa TSD Wilaya ya Wanging'ombe Bi.Rukia Mwelelwa Amesema Wanashindwa Kuwafuatilia Walimu Wanaotuhumiwa Kutenda Makosa Hayo Kutokana na Serikali Kushindwa Kuwapa Fedha za Kufanyia Uchunguzi wa Kesi Kama Hizo.

Katika Hatua Nyingine Walimu Wakuu Wamepewa Siku Saba Kuhakikisha Wanafunzi Ambao Hawajaripoti Shule Hadi Sasa Wanaripoti na Kuanza Masomo ya Kidato Cha Kwanza Haraka Iwezekaavyo.

Baadhi ya Wakuu wa Shule Hizo na Wenyeviti wa Kamati za Shule Hizo Wameeleza Baadhi ya Changamoto Ambazo Zinapaswa Kupatiwa Ufumbuzi Ikiwemo Kuwapa Motisha Walimu Katika Shule Zao.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles