UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI Arusha KUFANYIKA KESHO Julai 14.
 ![]()

 Mkurugenzi wa jiji la Arusha Sipora Liana akiwa anaongea na waandishi wa habari kuhusiana na uchaguzi wa udiwani jijini hapa

 picha chini na juu waandishi wa habari wakiwa wanasikiliza mkurugenzi wa jiji la Arusha

Halmashari ya jiji la Arusha inatarajia kufanya uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata nne za jijini hapa ambazo ni Elerai ,Kaloleni ,Kimandolu pamoja na Themi mnamo july 14 mwaka huu uchaguzi huu mdogo unafanyika kutokana na kuairishwa kwa uchaguzi mdogo wa kata hizi katika jimbo la Arusha mjini kutokana na sababu za kiusalama.
Akiongea na waandishi wa habari mkutugenzi wa jiji la Arusha Sipora Liana alisema kuwa uchaguzi huo uliarishwa kutokana Juni 16 kutokana na mabomu yaliyopigwa siku moja kabla ya uchaguzi na mungine ukaarishwa mapema juni 30 kutokana na kutojiridhisha kwa hali ya usalama iliyokuwepo katika jiji la Arusha.
Alisema kuwa kwa sasa maandalizi yaote yamekamilika na taratibu zote za kutangaza tena kwa wasimamizi ,wasimamizi wasaidizi pamoja na makarani zimekamilika na pia wameshapatiwa mafunzo kwa ajili ya wasimamizi hawa yameanza jana na yataendeshwa kwa muda wa siku tatu.
Aliwataja wagombea kutoka kata ya Kimandoku ni pamaja Edna Saul (CCM) pamoaja na Rayson Ngowi kutoka (CHADEMA) ,aidha alisema kuna jumla ya vituo 136 vya kupigia kura ambapoalisema kaloleni kuna vituo 27,elerahi 55,kimandolu 39, na kata ya themi vituo 15 .
Alisema kuwa jumala ya wapiga kura sitini elfu mia moja ishirini na tatu (60,123)wanatakiwa kupiga kura kaloleni itakuwa na wapiga kura 12,636,Elerai watakuwa wapiga kura 23,797,kimandulu 17,294 na Themi wapiga kura 6,396 aidha alisema kuwa wapiga kura wote wanatakiwa kufika katika vituo mapema kwani kura zitaanza kupigwa kuanzia saa moja asubui hadi saa kumi jioni ambapo baada ya hapo watafunga na askari watakuwa wanalinda vituo vyote.
Aliwataka wananchi kutimiza wajibu wao wa kupiga kura kwani zoezi hili ni muhimu huku akiwahakikishia kuwa usalama utakuwepo wa kutosha wakati wa kupiga kura na aliwataatharisha wananchi kuwa endapo mtu yeyete atawasumbua wakiwa katika eneo la kupigia kura watoe taarifa kwa askari aliopo karibu yake ili achukuliwe hatua za kisheria.
''ninawaomba kutowazingatia wanaopita kuwaaambia msijitokeze kwenda kutumia haki yenu ya msingi za kikatiba kuwachagua viongozi wenu pia napenda kuchukuwa nafasi hii kuwatakia wananchi wote wa jiji wa arusha uchaguzi mwema''alisema Sipora.