Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

KURA ZA MAONI KUPIGWA KESHO LUDEWA CCM[UBUNGE]

$
0
0
http://1.bp.blogspot.com/-2ydGo1snQ8Q/UGME6iQQQpI/AAAAAAAAEEc/KMdSDuANxLU/s1600/NEC+DOM+SEPT+25,+2012.jpg
 

Na Gabriel Kilamlya Ludewa

 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ludewa Kesho Wanatarajia Kupiga Kura Ili Kumchagua Mgombea Ubunge Atakayekwenda Kupambana na Vyama Vya Upinzani Katika Kupeperusha Bendera ya Chama Hicho Katika Nafasi ya Ubunge.

Akizungumza na MTANDAO huu Katibu wa CCM Wilaya ya Ludewa Bwana Lusiano Mbosa Amesema Kuwa Mchakato Kwa Ujumla Unaendelea Vyema Tangu Kutangaza Tarehe ya Kuchukua Fomu Hadi Kurejesha Ambapo Wagombea Wote  Kumi Ndani ya Chama Hicho Waliochukua Fomu Hizo Wamefanikiwa Kurejesha Tayari Kwa Upigaji Kura Hapo Kesho.

Hatua Hiyo ya Upigaji Kura Hapo Kesho Inakuja Kufuatia Kifo Cha Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo Hilo Kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Marehemu Deo Filikunjombe Kufariki Kwa Ajali ya Ndege Huko Katika Pori la Hifadhi ya Wanyama Serous.

Bwana Mbosa Amesema Kuwa Chama Cha Mapinduzi  Kinaelekea Katika Zoezi la Uchaguzi Kikiwa Bado na

Majonzi ya Kumpoteza Kiongozi Wa Wananchi Aliyekuwa Akipigania Maendeleo ya Wananchi na Msaada Mkubwa Kwa Jamii Huku Akiendelea Kuamini Wagombea Wote Kumi Waliofanikiwa Kurejesha Fomu.

Akizungumzia Ushindani wa Kisiasa Katika Jimbo Hilo Amesema Haamini Kama Kuna Upinzani Kwani Chama Hicho Kimejiimarisha Vya Kutosha Kuweza Kutwaa Jimbo Hilo.

Mara Bada ya Kupigwa Kwa Kura za Maoni Ndani ya CCM Ndipo Majina Yatapelekwa Kamati Kuu Ili Kurejesha Jina Moja Litakalo Kwenda Kushindanishwa na Mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Pamoja na Mambo Mengine Lakini Mwanahabari Wetu Toka Ludewa Amefanya Mazungumzo na Katibu Huyo Juu ya Maandalizi ya Mkutano Huo Ambapo Amesema Hadi Sasa Zoezi Limekwenda Vyema.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles