Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

NJOMBE PRESS CLUB YAWAKUTANISHA WADAU WA HABARI

$
0
0
wadau na waandishi wa habari wakisikiliza mada katika mkutano uliowakutanisha wadau wa habari mkoani njombe katika ukumbe wa fm hotel kujadili haali ya uchaguzi mwaka huu

mhasibu wa njombe press club Bwana Sunday Bavuga akiuliza swali kwa watoa ufafanuzi kuhusu uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyikaoktoba 25 mwaka huu

Mkalimani wa Watu Wasiosikia na kuongea Mkoani Njombe
Katibu Mtendaji wa Njombe Press Club Bwana Hamis Kasapa
waandishi wa habari kutokavyombo vya habari mbalimbali vilivyopo mkoani njombe ,waandishi binafsi wamitandao pamoja na wadau wakisikiliza mada katikamkutanouliowakutanisha wadau wa habari mbalimbali na waandishi wa habari mkoani humo katika kuchanganuoaa  mambao muhimu kuelekea uchaguzi mkuuu

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Njombe na Mgeni Rasmi Bwana Gedion Mwinami Akihutubia Katika Mkutano Huo.
mgombea wa ubunge njombe mji wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema Bwana Emmanuel Masonga  akitoa neno katika mkutano huo wa wadau

Mmoja wa watu kiziwi Mkoani Njombe Akiuliza maswali kwa mratibu wa uchaguzi mkoa wa Njombe


mwandishi na mtangazaji wa kituo cha redio greeni fm 91.5 Mhz iliopo wilayani makete mkoani njombe kijiji cha tandala kata ya tandala bw.henricky idawa naye
akisikiliza nini kinaendelea katika mkuano huo

mwenyekiti wa club ya waandishi wa habari mkoani njombe messy sekabogo akiwahsukuru wadau na waandishi wa habari walikubali kushirika mkutano wa wadau wa habari kuelekea uchaguzi mkuu

mmoja ya waandishi wa kituo cha redio mkoani njombe akiuliza swali kwa msimamizi wa uchaguzi

msimamizi wa uchaguzi mkoa wanjombe akitolea ufafanuzi juu ya namna uchaguzi utakavyoendeshwa ,kuanzia kampeni ambazo zinaendelea ,upigaji kura na kutangazwa matokeoNa Gabriel Kilamlya NJOMBE


Imeelezwa kuwa matumizi mazuri na sahihi ya kalamu kwa wanahabari katika mchakato wa Uchaguzi mkuu Nchini ndio njia pekee itakayoliweka Taifa sehemu salama katika zoezi hilo muhimu .


Kauli hiyo imetolewa na kaimu katibu tawala Mkoa wa Njombe bwana Gideon Mwinami wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa habari Mkoani Njombe ulioandaliwa na chama cha Waandishi wa habari mkoa huo(Njombe Press Club) chini ya ufadhili wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Nchini Tanzania UTPC.


Bwana Mwinami amesema kuwa kuzingatiwa kwa kanuni, sheria na miiko ya uandishi wa habari katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu  kutasaidia zoezi hilo liweze kwenda vizuri kwani hakutakuwa na uchochezi wala upendeleo kwa baadhi ya vyama vya siasa.


Hilmar Danda ni mratibu wa uchaguzi na mwanasheria toka ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye Amesema hadi sasa maandalizi ya vifaa vitakavyotumika siku ya kupiga kura yameshakamilika na bado mambo machache ambayo Hume yenyewe bado haijatoa muongozo.


Aidha bwana Danda amesema kuwa tume haikotayari kuona amani inatoweka katika mchakato huo eti kutokana na chama fulani kutaka kubebwa.


Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Njombe bwana John Temu Amesema jeshi la polisi limeimarisha na litaendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kuwekka doria katika kila eneo na vituo vya uchaguzi siku ya uchaguzi.


Taarifa ya chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe iliyosomwa na katibu wa chama hicho bwana Hamis Kassapa imevitaka vyombo vinavyohusika na zoezi hilo hususani Jeshi la polisi na tume ya Taifa ya uchaguzi kutenda haki katika mchakato huo ili kuepusha lawama dhidi ya vyombo vya habari.


Baadhi ya wanasiasa walioshiriki mkutano huo akiwemo mgombea ubunge jimbo la Njombe kusini kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema bwana  Emmanuel Masonga na mwakilishi wa chama cha mapinduzi ccm Anold Mtewele wametumia fursa hiyo kuvitaka vyombo vya habari kutenda haki katika kampeni hadi uchaguzi mkuu ili kuepusha adha inayoweza kujitokeza.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles